• December 27, 2024

Mto Wa Mauti

Hali ya taharuki na huzuni imetanda katika eneo la Gatoto baada ya kutambulika miili miwili ya wanaume mchana wa leo.Kwa mujibu wa wafanyi biashara karibu na daraja la Gatoto kwenye barabara ya Enterprise ni kwamba, waliona kitu kikiwa kimening’inia na wakadhani huenda ulikuwa mzoga wa nguruwe.

Hata hivyo, baada ya upekuzi, wamebaini ni mwili ulikuwa umeelea majini sehemu ya chini ya daraja hilo.Mita chache kutoka eneo hilo, vilevile pameshuhudiwa kitu kilichofanana na mzoga wa nguruwe, lakini baadaye ikabainika ulikuwa ni mwili wa binadamu.

Akidhibitisha visa hivyo, ocpd wa kaunti ndogo ya makadara timon Odingo amekieleza kituo hiki kwamba huenda mauaji yalitekelezwa kwingineko na kutupwa majini, ila ikasombwa hadi eneo hilo na maji ya mvua kubwa ambayo imeshuhudiwa katika siku chache ambazo zimepita.

Mwili mmoja ulikuwa na jeraha kichwani, huku wa pili ukiwa umefunikwa na nguo ambayo mwathiriwa wa pili alikuwa amevalia, hii ikiashiria wawili hao huenda waliuawa. hii ni kwa mujibu wa Odingo.


miili hiyo imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya city, huku uchunguzi ukianzishwa ………..

Script by Alomba Mercy.

published by Ledira Botere//DigitalSpace

Read Previous

RADIO REPORT

Read Next

FALSE: THE GOVERNMENT HAS NOT CANCELED THE HELB LOAN

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular