• September 13, 2024

 WORLD RADIO DAY 2020 (UMOJA WETU NGUVU YETU.)

Tangu jadi kabla ya wazinduzi wa teknoalojia hawajavumbua simu ilikuwepo radio. Kabla na baada ya kupata uhuru wakenya walitegemea sana radio kwa matangazo ili kuwakumbusha na kuwafahamisha kilichokuwa kikijiri. Kwa kifupi nitakuambia kwamba radio ni chombo cha mawasiliano kunachowafikia watu wengi zaidi ata kwa sasa tunapoishi kwenye ulimwengu uliotawaliwa na teknolijia na mitandao ya kijamii. 

Zipo runinga simu, majarida na magazeti lakini hakuna iliyozidi radio. Hii ndio maana katika kalenda ya umoja wa mataifa kila tarehe 13 feburuari ni siku kuu ya kusherekea radio ulimwenguni. Kila mwaka tunaposherekea siku hii huwa tunaongozwa na kibwagizo au mahudhui ya mwaka na mwakuu ikiwa ni kueka utofauti miongoni mwa jamii yaaani ‘Radio and Diversity’ ukilegeza ulimi.

Kwa muda mrefu radio imechangia pakubwa katika kuhamasisha na kuleta uiano na utangamano katika jamii. Baada ya machafuko yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, serikali iliunda tume iliyotwika jukumu la kuhakikisha kuna utengamano nchini NCIC, tume inayotambulika kisheria.

Katika kitongoji cha Mukuru inaishi jamii inayofahamu maana ya kutangengamana wakiweka kando tofauti zao za kikabila, kisiasa, kipato na kitabaka na kuja pamoja wakifahamu fika kuwa umoja ni nguvu na utengamano ni udhaifu. Hili halijaafikiwa pasi kuwepo radio, kituo cha Ruben Fm kinachopeperusha matangazo yake kwa jamii ya Mukuru kukichangia pakubwa huku kikiongozwa na kauli mbiu ya ‘Unganisha Jamii’ ili kuwaleta wanamukuru pamoja.

Correspondence:

Zephania Ingati amekuwa mkazi wa Mukuru kwa miaka 17 sasa na anafahamu wazi mchango wa kituo hiki tangia kuzinduliwa kwake Novemba 2016

Insert:

Intro; Ruben Fm imeunganisha watu, wazee kwa vijana, wamama kwa wasichana, Watoto kwa watu wazima…

Outro; Hata tumejuana watu wengi sana kupitia Ruben Fm.

Aidha Bw Ingati ameongezea kwamba biashara nyingi humu  mukuru vimeweza kuimarika huku akitupa kumbukumbu kuhusiana na na uchaguzi wa mwaka 2017 na jinsi hali ya utilivu iliweza kuimarishwa kuanzi kwa polisi hadi kwa wanasiasa.

Insert:

Intro; 2017 wakati wa siasa hakukuwa na rabsha humu Mukuru…

Outro; Kutangaza hata biashra yangu kwa Ruben Fm unapata wateja wanapata services zangu kwa urahisi.

Panapokuwa na jamii zaidi ya moja, tuambiane ukweli sharti pawe na tofauti lakini la muhimu ni jinsi wahusika wakuu watakapo hakikisha tofauti hizi zinamanufaa na hazizai hasira au vurugu.

Correspondence:

Rose Asena ambaye ni mwanaharakati kwa miaka 10 ambaye pia ni mkazi wa Mukuru na anafahamu umuhimu wa radio na jinsi kituo cha Ruben Fm kimefaa Mukuru. Asena anaelezea changamoto ambazo walipitia awali kabla ya ujio wa radio ya kijamii katika eneo hili la Mukuru 

 

 

Insert:

Intro; Pale nyuma kidogo uuh, it was very hard. Because ukiangalia distance from here mpaka mahali KBC Radio iko, it is a long distance, it requires someone to have money, ndio aweze kufika pale…

Outro; Am lacking words to describe what Ruben Fm is doing in our community.

Aidha Asena ameelezea baadhi ya manufaa ambayo yeye na wanaharakati wenza wamenufaika na radio ya kijamii huku akiwataka wawekezaji kuekuza zaidi katika radio za kijamii kwani zinachangia pakubwa katika kuwemo kwa amani miongoni mwa jamii.

Insert:

Intro; Personally it has helped me to grow, because aah, most of the time if you are a public figure, you find that most people want to interact with you…

Outro; Any apparatus that is working on peace building, should be embrassed and invested in.

Ghasi na vita vinahistoria yake. Kuna watu wanaochangia ili wafaidike kwa njia moja ama nyingine na wanapopanga kuanzisha mtafaruku huwa wanalenga sana vijana. Mwaka wa 2017 joto la kisiasa lilipanda nchini na mtaa wa Mukuru ukatajwa moja wapo ya mitaa iliyoshukiwa kushuhudia ghasia za baada ya uchaguzi. Ruben Fm ikasimama kidete ikaunganisha jamii iliyokuwa ina nyufa. Kwa mshangao wa wengi hakuna lilitokea.

Correspondance:

Hezbon Bahati ni mmoja wa viongozi wa vijana chini ya shirika la Mukuru Community Justice Centre ambalo linalojihusisha na kuhubiri amani Mukuru, mafunzo kwa vijana kuhusiana na jinsi ya kuanzisha miradi ya kujikimu kimaisha na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo maswala mengine katika jamii. Bahati anaelewa vizuri jinsi kituo hiki kilieneza amani miongoni mwa vijana na kubadili fikra za wengi wa vijana humu Mukuru wakati kulikuwa na joto la kisiasa nchini huku nchini ikielekea katika uchaguzi mkuu.

Insert:

Intro; Nikiangalia way back in 2017, tulikuwa na election na kulikuwa na mshikemshike, kulikuwa na hofu kwamba huenda tunaeza rudia vile 2007 ilihappen…

Outro; Walikuwa wanakuja kwa ground na wanachukuwa views za watu about ni nini inaendelea n ani nini wanaezataka ifanyike na how can we prevent people from getting back to 2007.

Aidha Bahati amesifia baadhi ya mijadala ambayo kituo cha Ruben Fm kimekuwa kikiwapeperushiwa wasikilizaji ambayo amesema imeweza kubadili dhana za msikilizaji huku akiongezea kwamba visa potovu vimeweza kupungungua kwani wahusika kuhofia kuanganziwa…

Insert:

Intro; Rates za violence zimepungua sana coz watu pia wamekuwa wakiogopa kuanikwa…

Outro; Hizo program ziko educative unaoana… unlike tu vile tunaweza  tuende maybe mtaani tufanye forum, hapa kwa radio mtu anakusikiza. Mtu anaweza kuwa anaosha vyombo lakini earphone iko kwa masikio, kuna program iko kwa background analearn unaona.

Conclusion.

Msikilizaji, niruhusu niseme hivi, ni wajibu wa radio kuhamasisha na kuchangia katika kuleta umoja na utangamano miongoni mwa jamii ila ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha ndoto hii inaafikiwa hapo ulipo na pembe zote za taifa. Tukubali kwamba tunaishi na makabila tofauti, na watu ambao mila zao na desturi zinakinzana la muhimu hapa ni wewe kuheshimu anachoamini mwenzako bora tu hakikudhuru. Tunaposherekea siku kuu ya radio ulimwenguni kibwagizo mwaka huu kikiwa ni Umoja Wetu Nguvu Yetu tuzidi kuungana tueneze amani, uiano, marudhianao na utengamano miongoni mwa jamii. Jina langu ni Moruri Denson, kwaheri.

 

Read Previous

NO MORE INTERNATIONAL EVENTS FOR KENYANS UNTIL FURTHER NOTICE.

Read Next

Harambee Starlets kuwania ubingwa wa dimba la Turkish Women Cup.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular