• November 21, 2024

MAKALA YA MADHEHEBU YENYE UTATA MUKURU

Karibu msikilizaji kwenye Makala ya madhehebu yenye utata hapa eneo la mukuru, jina langu ni ledira botere. Dini imeonekana kama kitu ambacho kinazidi kuenziwa tangu jadi na Madhehebu mengi kwa muda yanaonekana kuongezeka huku yale ya zamani yakiwa kidete na kuzindi kuimarisha mitindo yao kila kuchao.

madhehebu tofauti  huwa yamejengwa kwenye misingi tofauti huku baadhi ya misingi hiyo ikiwa toba, imani, ubatizo, kuwekea mikono, ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. Imani kwenye madhehebu haya imeonekana  kuwa kitu ambacho kinazingatiwa kwa kina.je imani ni nini?  kulingana na bibilia wahebrania mlango wa kumi na moja imani ni ule uhakika wa mambo yatarajiwayo au bayana ya mambo yasiyoonekana,kwenye dini ya kiislamu ni utambuzi wa muumini katika imani na matendo katika nyanja za kidini za Uislamu.kulingana na ufafanuzi huu imani hujengwa kutokana na matendo tofauti ambayo washirika tofauti huamini na kudhihirisha.

Hapa eneo la mukuru kwa reuben tunaangazia upekuzi wa dhehebu la reformed United Cross Church of Africa ambapo Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa mafunzo na Imani tata hali hii imeleta tumbo joto huku wakaazi wengi wakitoa hisia zao kulingana na mienendo na itikadi za dhehebu hili.

Kutokana na madai haya, niliweza kutafuta wafuasi wa dini hii na waliweza kutoa hisia zao kulingana na madai haya….

Hata hivyo  Muuguzi mmoja  katika hospitali ya Ruben Health Centre ambaye tumelibana jina lake kwa usalama wake, alikumbana na kisa kimoja ambapo mshirika wa kanisa hili tata aliletwa na wahudumu wa afya wa hapa mukuru yaani CHV kwa nguvu  baada ya kukataa kwenda hospitalini. Anazidi kutuelezea nini hasa kilitokea kwa kina……

Juhudi zetu za kutaka kujua kama kweli dhehebu hili la reformed United Cross Church of Africa lina funza itikadi kama hizi ziliweza kufua dafu kwani kiongozi ambaye ametwikwa jukumu la eneo hilo la rurii B bw. Kaloki aliweza kuwaandikia barua rasmi viongozi wa dhehebu hili  na kuwaalika kwenye kikao kwenye ofisi ya chifu wa eneo hili mnamo tarehe mbili mwezi Aprili mwaka wa 2023 ili waweze kufafanua kwa kina iwapo madai haya ni ya kweli au la….

Ni bayana kuwa kila mwamba ngoma anavuta kwake maanake baadhi ya wakazi wanalalamikia itikadi kali na uovu unaoendelezwa kwenye kanisa hilo huku Mchungaji akikana madai hayo. Hivi ni nani atakayeingilia kati na kuhakikisha kuwa wakazi hawapitii hadaa za kidini? Na je, mafunzo na doktrini za Biblia zinasemaje kuhusu manabii wa uongo?

Hata hivyo wakazi  wa eneo hilo la rurii b wamewarai viongozi na wahusika wanaodhibiti maswala ya kidini kuingilia kati na kuwapa usaidizi unaofaa…..

Swali ni je iwapo imani ya mshirika wa dhehebu hili itamzuia kuenda hositalini nani anafaa kushughulikia maswala ya afya  kwenye dhehebu hili na je anayefunza imani hii ni nani???

Nikiripotia ruben fm jina langu ni ledira botere.

Read Previous

World Press Freedom Day 2023

Read Next

Ajira ya Watoto Eneo la Mukuru kwa Ruben

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular