• December 24, 2024

MAKALA YA SHERIA UNAPOSHIKWA NA POLISI

KARIBU MSIKILIZAJI KWENYE MAKALA YA SHERIA UNAPOSHIKWA NA POLISI…JINA LANGU NI LEDIRA BOTERE….

Kila kuchao kuna uwezekano wakujipata kwenye upande mbaya wa sheria na mara kwa mara watu wengi hujipata korokoroni bila ya kujua sheria za kwalinda au za kuwawezasha  kujitetea wanapojipata katika mazingira haya.

Wakazi wengi Katika eneo la mukuru wanazidi kutoa hisia zao za iwapo sheria kama hizi wanazijua almaarufu miranda rights kwa lugha ya kimombo na wakati wanapokumbana na mkono wa sheria iwapo  zinatiliwa maanani na wale ambao wametwikwa jukumu la kulinda sheria hizo

hivi karibuni kumeshuhudiwa visa vya Kuzuiliwa kiholela  hapa mukuru kwa Reuben yaani kwa lugha ya kimombo arbitrary arrests maanake ni wakati mtu anakamatwa na kuzuiliwa na serikali bila kufuata utaratibu na bila ulinzi wa kisheria wa kesi ya haki, au wakati mtu anawekwa kizuizini bila msingi wowote wa kisheria wa kunyimwa uhuru.

Katika katiba ya nchi kuna vipengee kadha kwenye mswada wa haki yaani bill of rights, mfano kipengee kama cha 49 ndani ya katiba ambacho kinasema Mtu aliyekamatwa ana haki– kufahamishwa mara moja, kwa lugha ambayo mtu huyo anaielewa, kuhusu– sababu ya kukamatwa; haki ya kukaa kimya; namatokeo ya kutonyamaza. Bi Roseline asena ni mwanasheria wa kijamii anazidi kunifafanulia kwa kina sheria hizi……

 

Swali ibuka likiwa ni je wajua haki zako unaposhikwa hapa mtaani?

 

Makala haya yameletwa kwako na ruben fm, kwa hisani ya Edmund Rice Foundation Australia (ERFA) mimi ni mwandalizi wako ledira botere

 

Read Previous

WORLD RADIO DAY RUBEN FM

Read Next

UCHAFUZI WA HEWA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular