• December 26, 2024

Jinamizi La Takataka Katika Mtaa Wa  Mukuru

 

Licha ya serikali ya Kenya Kwanza Kuweka mikakati ya kujizatiti katika shughuli za kuhifadhi mazingira, bado sehemu nyingi zinakumbwa na changamoto nyingi katika swala hili.

Hii  inadhiirishwa wazi katika mtaa wa Mukuru unaopatikana katika eneo bunge la Embakasi Kusini.

Sehemu nyingi  zimetapakaa taka  hasa katika barabara  na mitaro. Hii inaazidishwa  na mvua  inayo endelea kunyesha ambayo husomba takataka nyingi na kuziweka katika mitaro na barabara.

Mtaa huu wa Mukuru una idadi ya watu wengi. Kujaa huku kwa taka kuna weka hatari ya kuweza kuleta mlipuko wa magonjwa katika eneo hilo. Nilizungumza na baadhi ya Wakaazi wa hapa, katika harakati ya kutaka kuyapata maoni yao kuhusu swala hili la Taka. Wengi walikasirishwa na jinsi swala hili la ukusanyaji wa taka  jinsi halijatiwa mkaazo, hasa Zaidi na uongozi wa Kaunti ya Nairobi, Kwani utapakaji huu wa taka ina ipatia taswira mbaya eneo hilo.

Dennis Mbito ambaye ni mhudumu wa boda boda anasimulia. “ Jambo hili la takataka katika mtaa huu ni swala nyeti sana. Yani kujaa kwa takataka katika mtaa huu, kumekuwa tu kama jambo la kawaida tu. Yani kila sehemu ni takataka tu. Mimi ningekuwa na mapato mazuri naeza kutafuta maeneo ambayo ni safi”. Anasema ikiwa mikakati ya kuusafisha mji huu, basi linaeza kuwa jambo murua kabisa.

Kaunti ya Nairobi chini ya usimamizi wa gavana Johnson Sakaja, ilianzisha vuguvugu la ‘’ green movement”. Vuguvugu hili ambalo linajumuisha idadi wengi ya vijana, linajukumu la kusafisha mji wa Nairobi na viunga vyake. Lakini Katika pitapita zangu, sijaona mhudu yeyote wa vugugu hilo katika mtaa huu wa Mukuru kwa Ruben.

Shirika la umoja wa kimataifa, limekuwa likitilia mkazo zaidi kuhusu uwekaji wa mazingira safi duniani, hasa katika vita dhidi ya Tabia nchi. Hoteli nyingi zinaendelea kuhudumu licha ya kuwa karibu na takataka. Hii ni hali hatari kwa afya.

Mwanabiashara wa Hoteli ambaye tutambandika jina John, kwani jina lake tumelibana kwasababu hakutaka kutambuliwa jina, anasema Wateja wengi hawafuraishwi na kuweka hoteli karibu na takataka, kwani baadhi yao huenda baada ya kuona takataka zikuwa zimetapakaa. “Biashara yangu ingenoga sana ikiwa takataka hizi zingekuwa zinatolewa, baadhi ya wateja wangu wako very sensitive sana na mambo ya usafi” Anasema John, si kwake tu pekee, kwani hali ni ile ile katika maeneo mengi ya mtaa huu.

Lakini licha ya hali  hii kuendelea,  Shirika la CBO gateway la Kujitolea, ambalo wanachama wao wengi ni vijana, huwa linaweka mikakati ya kusafisha mtaa huu. Ingawaje wanakumbwa na uhaba wa fedha za kuendeleza shughuli hii ya usafishaji. Kiongozi wao Mike Mwangi, Anawasihii wafadhili  kuwa unga   kwa kuwapa fedha ambazo zinaweza kuwafadhili kununua vifaa vinavyo stahili kuundeleza shughuli hii yao ya usafishaji.

Bila shaka swala la takataka, linazidi kuwa kizungumkuti  hasa katika eneo hili la Mukuru. Wakaazi wana matumaini kwamba, serikali itaweza kuweka mikaati ya uondoaji wa takataka katika eneo hili.

Ruben Fm jina langu ni Bob Kau.

 

Read Previous

Christian community on matters affecting the community

Read Next

UHABA WA MAJI KATIKA ENEO LA MUKURU KWA REUBEN

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular