FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyochapishwa jana tarehe 17 Agosti imeweka Mfuko wa Maendeleo ya Maeneo Bunge (CDF) wa Embakasi kusini chini ya darubini. Kulingana na matokeo, jumla ya shilingi bilioni 4.1 zipo katika mashaka kote nchini, huku Embakasi kusini ikitajwa kwa kuwa na sakata ya shilingi milioni 91.9 ambazo hazijulikani matumizi yake, hasa kutoka mgao wa bursari. Ripoti hiyo imeibua wasiwasi miongoni mwa wakazi na nalivalia njuga swali kubaini iwapo wakazi hawa wanapata hizi basari na kwa njia ipi
Wakazi wanasema mchakato wa bursari katika Embakasi kusini umejaa usiri na upendeleo na wale walio na uhusiano wa karibu na viongozi wa eneo au watu wenye ushawishi ndio wanaopata mgao wa bursari, huku familia nyingi zenye uhitaji mkubwa zikiachwa nje. Adha Wazazi wanalalamika kwamba licha ya kuwasilisha nyaraka zote zinazohitajika, maombi yao hupuuziwa au hukataliwa bila maelezo yoyote.
Shida nyingine iliyotajwa na jamii ni uuzaji wa fomu za bursari, ambazo kimsingi zinapaswa kutolewa bure. Wanakijiji wanadai kuwa fomu hizo zinauzwa kwa viwango tofauti, kuanzia shilingi 2000 hadi 3000, kutegemea ni nani unayemfuata. Wanasema hii inaongeza mzigo wa kifedha kwa familia zinazohangaika, ambazo nyingi haziwezi hata kumudu mahitaji ya msingi ya shule.
Jamii sasa inataka kuwe na uwazi na uwajibikaji mkubwa zaidi katika usimamizi wa CDF. Wanadai kuwa rekodi za mgao wa fedha ziwekwe wazi, uchunguzi ufanyike kuhusu uuzaji wa fomu za bursari, na kuwe na mifumo madhubuti ya usimamizi ili kuhakikisha watoto wenye uhitaji wanasaidiwa. Kwa kuwa elimu ndiyo njia pekee ya kuondokana na umasikini kwa wengi Mukuru, Kwao, bursari ilipaswa kuwa msaada wa kweli wala siyo mzigo wa ziada. Ni Makala ya uwazi wa basari hapa Embakasi kusini jina langu ni ledira Botere, Ruben FM