• March 16, 2026

MAFURIKO RURII

Wakaazi wa eneo la Rorie B hapa mtaani walitatizika Jumamosi usiku, wengi wakilazimika kukesha wakiondoa maji kwenye nyumba zao.

Kulingana na walioathiriwa, licha ya kwamba mvua hazikunyesha maeneo haya, mafuriko yalishuhudiwa kuanzia saa sita usiku, huku nyumba nyingii zikifurika.

Ilielezwa baadaye kwamba mafuriko hayo yalitokana na mto Ngong kuvunja kingo zake na kupelekea maji kusambaa maeneo hayo.

Ni mmoja wa waathiriwa akieleza masaibu waliyokumbana nayo usiku wa kuamkia Jumapili.

Licha ya mvua kukosa kunyesha maeneo haya, mafuriko makubwa yalishuhudiwa huku wenyeji wakilaumu mfumo mbaya wa kupitisha maji taka.

Meneja wa shule ya Bridge International Dan Wamalwa vile vile ametaja baadhi ya changamoto zinazoathiri eneo hilo.

Wakati uo huo, wenyeji wamelalamikia kile wameeleza kuwa ni upendeleo wakati wa ugavi wa misaada kwa waatahiriwa, wakidai wengi hawafikiwi na misaada hiyo, badala yake wanaosimamia zoezi la usambazaji huwapa jamaa na rafiki zao wa karibu.

REPORT BY HABAKUK NGURE

Read Previous

POLICE GENDER DESK OFFICERS AND SGBV CHAMPIONS ROUNDTABLE DISCUSSIONS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular