• August 21, 2025

Faida za kiafya za tangawizi

Faida za kiafya za tangawizi
Je,wajua kuwa tangawizi inaweza ikamaliza tatizo la kichefuchefu na kutapika? Ndio, kukula vyakula vilivyo na tangawizi,chai au biskuti kunaweza kukaondoa kichefuchefu asubuhi kwa wajawazito,kuondoa kichefuchefu cha safari au cha baada ya kufanyiwa upasuaji.

Faida zingine za kiafya za tangawizi ni kama zifuatazo;
~Husaidia kupunguza gesi na kiungulia kwani husababisha mate na juisi za tumbo kuachiliwa kwa haraka ili chakula kisiagwe na kumeng’enywa vizuri.

~Hupunguza maumivu na uvimbe mwilini kwani ina gingerols ambazo ni kemikali za asili za kupunguza uvimbe na maumivu mfano wa misuli au ukiwa na arthritis.

~Tangawizi huimarisha kinga ya mwili kwani iko na viambato vinavyopambanana vijidudu na virus, hivyo kusaidia mwili kupambana na magonjwa yanapoibuka.

~Husaidia kudhibiti sukari ya damu. Utafiti unaonyesha kuwa tangawizi husaidia kupunguza kiwango cha sukari na kuongeza unyeti wa insulini.

~Tangawizi ya moto au unga husaidia kupunguza maumivu ya hedhi. Kunywa chai moto ya tangawizi pindi tu unapohisi maumivu siku za hedhi.

~Tangawizi husaidia kupunguza kiwango cha cholesterol na kusaidia mzungumo mzuri wa damu hivyo kulinda afya ya moyo wako.

~Tangawizi ina antioxidants ambazo husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya ubongo na hukinga seli za ubongo dhidi ya uharibifu.

Kumbuka;
Unaweza ukatumia tangawizi kwa vyakula,chai ya maziwa au kwa maji moto.
Usikule tangawizi nyingi sana kwani inaweza ikasababisha kiungulia au hata kichefuchefu.

Makala  haya yameandaliwa na Tabitha Njambi.

Read Previous

International Youth Day 2025

Read Next

🚨 Breaking News: Evening Fire Razes Homes in Kwa Rueben’s Diamond Area

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular