FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Visa viwili vya moto vimetokea ndani ya masaa machache eneo la Ruben katika maeneo tofauti ikiwemo iliyoripotiwa jana usiku huko Kosovo na ingine iliripotiwa leo asubuhi eneo la Bantu. Waathiriwa wa maeneo hayo wanasema wamepoteza mali zao na wanaomba msaada wa dharura kutoka kwa serikali.
Joseph Kaloki, mwenyekiti mkuu wa eneo la Ruben, amewahimiza wakaazi wasaidiane wakati huu mgumu kwa kuwa umoja ni nguvu. Vile vile Bw. John Orure, msaidizi wa kibinafsi wa MCA, amesema MCA anafahamu mkasa huo na atafanya mipango ya kutoa msaada kwa walioathiriwa. Pia ametoa wito kwa serikali na wahisani ili waweze kusaidia.
walioshuhudia tukio la usiku wa jana wamesema moto ulianza ghafla katika moja ya nyumba na kusambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali. Wakaazi walijaribu kutumia maji na mchanga kuuzima moto kabla ya magari ya zima moto kufika, lakini juhudi zao hazikuweza kuzuia uharibifu mkubwa.
Katika eneo la Bantu, moto wa asubuhi leo umewaacha familia kadhaa bila makazi. Baadhi ya walioathiriwa wamelazimika kuhamia kwa majirani na marafiki huku wengine wakitafuta hifadhi katika vituo vya jamii. Wamesema wanahitaji mavazi, chakula na vifaa vya kujikinga na baridi hasa kwa watoto wadogo na wazee.
Viongozi wa kijamii wameonya kuwa visa vya moto katika maeneo ya mabanda vinaongezeka kutokana na mfumo wa umeme usio salama, matumizi ya jiko za mkaa na gesi katika nafasi finyu, pamoja na miundo ya nyumba kuwa karibu sana. Wamewataka wakaazi kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari ili kuepuka majanga kama haya.
Shirika la Msalaba Mwekundu na mashirika mengine ya misaada yameombwa kuingilia kati haraka ili kusaidia kwa vifaa vya dharura. Wakaazi wamesema msaada wa haraka utasaidia kuokoa maisha, kurejesha heshima na matumaini kwa familia zilizoathirika.
Mamlaka husika zinatarajiwa kufanya uchunguzi wa chanzo cha milipuko hii ya moto ili kuhakikisha hatua za kuzuia matukio kama haya zinachukuliwa.
REPORT BY : ALICE ODERA