FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
CORRUPTION ON CDF 91.9 MILLION
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyochapishwa jana tarehe 17 Agosti imeweka Mfuko wa Maendeleo ya Maeneo Bunge (CDF) wa Embakasi kusini chini ya darubini. Kulingana na matokeo, jumla ya shilingi bilioni 4.1 zipo katika mashaka kote nchini, huku Embakasi South ikitajwa kwa kuwa na sakata ya shilingi milioni 91.9 ambazo hazijulikani matumizi yake, hasa kutoka mgao wa basari. Ripoti hiyo imeibua wasiwasi miongoni mwa wakazi na nalivalia njuga swali kubaini iwapo wakazi hawa wanapata hizi basari na kwa njia ipi
Wakazi wanasema mchakato wa basari katika Embakasi kusini umejaa usiri na upendeleo na wale walio na uhusiano wa karibu na viongozi wa eneo au watu wenye ushawishi ndio wanaopata mgao wa basari, huku familia nyingi zenye uhitaji mkubwa zikiachwa nje. Adha Wazazi wanalalamika kwamba licha ya kuwasilisha nyaraka zote zinazohitajika, maombi yao hupuuziwa au hukataliwa bila maelezo yoyote…….