• September 12, 2024

NYUMBA KUMI

Kwa muda, wengi haswaa katika mitaa ya mabanda wamekuwa na changamoto ya ni wapi wanapaswa kuripoti matukio katika jamii. Hata hivyo, hili lilirahisishwa kufuatia kubuniwa kwa mpango wa nyumba kumi, ambao ni macho ya serikali mashinani katika jamii.

Ni kutokana na hili ambapo Ruben Centre imeandaa kikao na baadhi ya wana nyumba kumi kutoka maeneo ya Viwandani, Mukuru kwa Ruben na Kwa Njenga, haswaa ikizingatiwa malalamishi ya mara kwa mara dhidi yao.

Mercy Alomba na maelezo zaidi.

Serikali ilianzisha mpango wa Nyumba katika jamii nchini kupitia Agizo la Rais mwaka wa 2013 lililolenga kuhakikisha vitongoji salama na endelevu kuhusiana na maswala ya usalama.

Licha ya kutambuliwa na serikali, takriban miaka kumi baadaye, changamoto zinazidi kuwasonga, kuu ikiwa ukosefu wa ajira, pingamizi kutoka kwa baadhi ya viongozi, anavyodokeza Eunicekutoka eneo la Feed The Children

Anatolea mfano wa kisa ambapo kutokana na changamoto za kinyumbani, mwanamke mmoja aliuza mtoto baada ya kujifungulia kwa mkunga.

Naye mwenzake kutoka Simba Cool ameunga mkono madai haya pia.

Future Mukiri naye ameeleza mtazamo wake kuhusiana na changamoto kuu ambayo lawama zimeelekezwa kwa wenye kiti.

Maggy Kariuki mshirikishi wa uhamasisho Ruben Centre ameeleza sababu zilizopelekea kuandaliwa kwa mkutano huu

Read Previous

BAADA YA DHIKI NI FARAJA

Read Next

Makala Maalum : CS Awareness Month 2023

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular