• December 26, 2024

WORLD SAFE ABORTION DAY

Kenya imejumuika na ulimwengu katika maadhimisho ya siku ya uavyaji mimba, mada ya mwaka huu ikiwa Utoaji mimba ni huduma ya afya, na afya ni haki ya binadamu.Ni siku ambayo imejiri huku kukiwa na midahalo kinzani kuhusu swala hili.Mwanahabari wetu Mercy Alomba ameangazia baadhi ya athari zinazojitokeza mwanamke anapoavya mimba kwa kutumia njia zisizo salama na kutuandalia makala yafuatayo………………UAVYAJI MIMBA, CHAGUO LANGU, HAKI YA KIBINADAMU…………..

………………EXPLANATION………….

NI ZULFA JUMA, ALIYEPONEA KUFA KUTOKANA NA ATHARI ZA KUAVYA MIMBA KUPITIA NJIA ISIYO SALAMA, AKIELEZA MASAIBU YALIYOMKUTA…..

JUMA NI MIONGONI MWA MAELFU YA WANAWAKE WANAOCHUKUA JUKUMU LA KUTOA UJA UZITO KUPITIA MLANGO WA NYUMA, KUTOKANA NA SHERIA TATA ZA HUMU NCHINI KUHUSU HAKI YA UAVYAJI MIMBA.

13% YA VIFO VYA WANAWAKE WAZAZI VINATOKANA NA UAVYAJI MIMBA USIO SALAMA NCHINI, KWA MUJIBU WA MATOKEO YA UTAFITI WA KITUO CHA UTAFITI WA IDADI YA WATU NA AFYA AFRIKA APHRC.

LAKINI NI MBINU ZIPI HIZI AMBAZO HUTUMIKA NA WANAWAKE?

KENNEDY JUMA, AFISA WA UTAFITI APHRC, ANAELEZA KUHUSU MBINU HATARI ZA UAVYAJI MIMBA, ZINAZOTUMIWA NA WANAWAKE WENGI NCHINI…..

…………………JUMA MBINU………………..

ANAFICHUA WENGI HUJUA MBINU HIZO NI HATARI, ILA WANAZIKUMBATIA TU….

………………JUMA USIRI………………..

HAKI YA AFYA NI HAKI YA KIMSINGI YA BINADAMU ILIYOHAKIKISHWA KATIKA KATIBA YA KENYA.  KIFUNGU CHA 43 (1) (A) CHA KATIBA KINAELEZA KILA MTU ANA HAKI YA KUPATA KIWANGO CHA JUU CHA HUDUMA ZA AFYA KINACHOWEZA KUFIKIWA, ILA PAMEKUWA HISIA MSOTE IFIKIAPO SWALA LA HAKI YA UAVYAJI MIMBA.

KIPENGEE CHA 26, SEHEMU YA NNE YA KATIBA KINATOA MWONGOZO KUHUSU VIGEZO VYA KUZINGATIWA KATIKA UAVYAJI MIMBA, IKIWA NI PAMOJA NA KATIKA JITIHADA ZA KUOKOA MAISHA YA MAMA.

KWA MUJIBU WA UTAFITI UNAOENDELEA WA APHRC KUHUSU UAVYAJI MIMBA NCHINI, KATI YA JULAI NA AGOSTI MWAKA HUU, WANAWAKE 4300 WALIFIKA KATIKA VITUO VYA AFYA 430 VYA HUMU NCHINI WAKISAKA HUDUMA ZA MATIBABU YA BAADA YA UAVYAJI  MIMBA.

KANDO NA ATHARI KWENYE MWILI WA MWANAMKE AU HATA MAUTI, INAGHARIMU SERIKALI KIASI KIKUBWA CHA FEDHA KATIKA KUGHARAMIA MATIBABU YA ATHARI ZA BAADA YA UAVYAJI MIMBA USIO SALAMA..

KENNEDY ANAFAFANUA HILI.

………………….KENNEDY COST…………………….

ANAFAFANUA GHARAMA YA MATIBABU HULINGANA NA VIWANGO VYA MAAFA…

………………….KENNEDY COMPLICATION……………..

LAKINI SHILINGI MILIONI 533 ZAWEZA KUFAIDI VIPI TAIFA IWAPO UAVYAJI MIMBA UTAKUWA NI HAKI YA KIMSINGI YA KIBINADAMU?

……………..KENNEDY SAVE…………………

KWA UPANDE MWINGINE, MCHUNGAJI MARTIN BUNYALI ANATOFAUTIANA NA PENDEKEZO LA KENNEDY…

……………..BUNYALI GOD……………………

ZULFA NAYE ANA MTAZAMO UPI KUHUSU UAVYAJI MIMBA KAMA HAKI YA KIBINADAM?

…………………..SAFE HUMAN…………………

NI ANTHONY AJAIYI, AFISA WA UCHUNGUZI WA SAYANSI APHRC, AKIWASILISHA MTAZAMO WAKE KUHUSIANA NA MDAHALO WA IWAPO UAVYAJI MIMBA UNAPASWA KUWA HAKI YA KIMSINGI YA AFYA.

……………………………ANTHONY AJAIYI……………

MSIKILIZAJI, HATA ULIMWENGU UNAPOADHIMISHA SIKU YA UAVYAJI MIMBA SALAMA, MADA YA MWAKA HUU KWA MUJIBU WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI WHO IKIWA UAVYAJI MIMBA NI HUDUMA YA AFYA, NA AFYA NI HAKI YA KIBINADAMU, NI TUMAINI LA WENGI KWAMBA PATAPATIKANA MWAFAKA, NA KILA MMOJA APATE HAKI  YA KUPATA HUDUMA HIZI PASI KUBAGULIWA, KUDHALALISHWA AU HATA KUHUKUMIWA.

Read Previous

VIKUNDI VYA USAFI MUKURU

Read Next

Athari za Tabianchi kwa walemavu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular