• April 14, 2024

Athari za Tabianchi kwa walemavu

Watu wenye ulemavu wana uwezekano wa kuaga dunia mara mbili hadi nne zaidi ya mtu wa kawaida au kujeruhiwa katika hali ya dharura , Zaidi ya hayo, watu wenye ulemavu katika misiba wanakabiliwa na changamoto za usafiri usiofikika na makazi ya dharura, kutengwa na jamii kwenye taasisi tofauti tofauti.

 

Mabadiliko ya hali ya hewa yaani tabianchi yanaongeza changamoto zinazowakabili watu wanaoishi na ulemavu ikiwemo kupunguza upatikanaji wa huduma za afya, chakula, maji na miundombinu isiofikika. Watu wenye ulemavu wa kisaikolojia na Ngozi wana mara tatu ya kiwango cha vifo katika mawimbi ya joto.

 

Changamoto hizi za watu wenye ulemavu zinashuudiwa kote ulimwenguni na huathiri sana  wale ambao wanaishi kwenye mitaa ya mabanda ikiwemo Mukuru ,korogosho , kibra , Soweto na meaneo mengine yenye mitaa hii kwani miundo mbinu mingi haijawafikia ipasavyo.

 

Katika eneo la mukuru kwa reuben najuinga na  kingozi anaye wakilisha walemavu kwenye shirika la watu wanaoishi na ulemavu yaani ncpwd nakuweza kutufafanulia kwa kina hasa ni changa moto zipi wanazo pitia hapa mtaaani hasa kutokana na tabianchi….

Hata hivyo mashirika mengi kwenye mitaa ya mabanda huwa mara kwa mara wanawasahau watu wanaoishi na ulemavu katika kuwahusisha kwenye miradi tofauti za utunzi wa mazingira.

Bw odongo kevin ambaye ni mwanzilishi wa green slum innovation hub anajitosa kwenye ulingo wa kuwasaidia watu wanaoishi na ulemavu huku akitoa changamoto zinazo wakumba walemavu eneo hilo.

Mbinu za kukabiliana na hali ya hewa iliyotengenezwa bila kushauriana na mashirika ya watu wenye ulemavu hujenga vikwazo vya ziada. Kwa mfano, njia za ziada za baiskeli zinaweza kusababisha vituo vya mabasi kushindwa kufikiwa na viti vya magurudumu, miundo mbinu pia huchangia pakubwa mfano nyumba.

Bw. Collins ombajo ambaye ni mwana harakati wa kutetea haki za watu wanaishi na ulemavu anazidi kunifafanulia kwa kina baadhi ya changa moto hizi na pia suluhishow kwa ujumla…

Kulingana na katiba ya nchi kipengee cha 54 inahitaji watu wenye ulemavu kushughulikiwa kwa njia isiyowadhalilisha. Haki hii inatetea kutobaguliwa kwa watu wenye ulemavu kwa misingi yoyote ile. Bw odongo anazidi kuwasihi washikadau tofauti kuajibika kwa kuwahusisha walemavu kwenye shughuli na mazingira kwa kuweka mikakati tofauti…

Makala haya ya watu wanaoishi na ulemavu kuhusishwa kwenye utunzi wa mazingira yameandaliwa na kuletwa kwako nami ledira botere .

Read Previous

WORLD SAFE ABORTION DAY

Read Next

DUMPING IN MUKURU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular