• December 27, 2024

UCHAFUZI WA HEWA

Katika miji inayoshuhudia ongezeko katika idadi ya watu na shughuli za viwandani na uzalishaji, hewa tunayopumua kwa wakati mwingi huchukuliwa na wengi kimzaha… lakini katika Maisha haya, kuna tishio la kimya, uchafuzi wa hewa.

Mercy Alomba na maelezo zaidi..

Wito umetolewa kwa waandishi wa Habari kuzingatia umuhimu wa kuripoti kwa uwajibikaji kuhusu uchafuzi wa hew ana athari zake kwa jamii.

Kwenye kikao cha siku mbili kilicholeta Pamoja mashirika mbali mbali ikiwemo Internews na wanahabari,

Swala la haja ya kuangazia uchafuzi wa hewa lilichipuka.

Purity Munyambo, afisa anayesimamia maswala ya kijinsia na athari za uchafuzi wa hewa dhidi ya jinsia mbali mbali  katika shirika la World Resource Institute akieleza athari za hewa chafu kwa wanawake, licha ya jinsia zote kuathirika.

Katika mtaa wa Mukuru kwa Ruben, wenyeji wameibua hisia mesto kuhusiana na swala nzima la uchafuzi wa hewa na athari zake.

Mshirikishi katika shirika la Internews Earth Journalism Network Daktari Jacky Lidubwi anaeleza haja ya wanahabari kuangazia zaidi kuripoti kuhusu hewa safi, kama njia moja ya kuhamasisha jamii, ila ameonya dhidi ya kuangazia mitaa ya mabanda kama inayoathirika na hewa chafu pekee.

Mtazamo wake Lidubwi umepigiwa upato, japo imeelezwa ni jukumu la kila mmoja.

Tulivyosikia, Kwa kuangazia tishio hili lisiloonekana, waandishi wa habari wana uwezo wa kuhamasisha hatua na kuleta mabadiliko chanya kwa afya na ustawi wa wote. Kumbuka, hewa tunayopumua inatuathiri sote – tuhakikishe ni safi na salama kwa vizazi vijavyo.

Read Previous

MAKALA YA SHERIA UNAPOSHIKWA NA POLISI

Read Next

UFUGAJI WA BLACK SOLDIER FLY

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular