• July 24, 2024

UFUGAJI WA BLACK SOLDIER FLY

Black soldier fly

Karibu msikilizaji kwenye makala ya kilimo biashara hapa mukuru jina langu ni ledira botere.

Hermetia ilucens, yaani black soldier fly kwa lugha ya kimombo, ni nzi wa kawaida na aliyeenea sana Tangu mwishoni mwa karne ya 20, na amekuwa akizingatiwa zaidi kwa sababu ya manufaa yake kwa kuchakata taka za kikaboni yaani organic waste na kuzalisha malisho ya wanyama na mbolea kwa mimea.

Black soldier fly ni inzi anayeiga kwa sana na, aliye karibu sana kwa kimo, rangi, na mwonekano wa nyigu wa matope ya bomba  yaani mud dauber wasp. Uigaji wa aina hii ya nyigu huimarishwa hasa kwa kuwa antena za inzi ni ndefu kama za nyigu, tarsi ya nyuma ya inzi ni ya rangi ya kijivujivu, kama ilivyo kwa nyigu, na  ana “madirisha” mawili madogo na ya uwazi kwenye sehemu ya chini ya fumbatio.

Kikundi cha ubuntu hapa eneo la mukuru kwa reuben, kimekuwa kikundi cha kuigwa na kutiliwa mfano kwani wameanzisha ukulima wa black soldier fly kama njia moja wapo ya kujiajiri na najuinga steve omondi ambaye ni mwenyekiti wa kikundi hiki na anazidi kunielezea kwa kina ni nini kiliwavutia kujinga na ufugaji huu…

FAIDA ZA INZI HAWA HUWA NYINGI SANA KWANI Mabuu yaani lavae ya black soldier fly hucheza jukumu sawa na la minyoo nyekundu YAANI RED WORMS kama watenganishaji muhimu katika kuvunja taka au vyakula za kikaboni na kurudisha rutuba kwenye udongo. Zaidi ya hayo, mabuu ya nzi hawa ni chanzo mbadala cha protini kwa ufugaji wa samaki, malisho ya wanyama na chakula cha mifugo, bwana Erick ambaye ni  Mtaalam kutoka taasisi ya kimataifa YA wataalamu wa kilimo miramar anazidi kutufafanunulia kwa kina faida za nzi hawa

Hata hivyo ni wazi kuwa kila aina ya kilimo biashara huwa na changamoto ya aina yake kama vile baadhi ya wanakikundi hiki cha ubuntu wanavyonielezea….

Aidha kikundi hiki kumewarai vijana hapa mtaani kujiunga na shughuli za kilimo biashara ili kuweza kuongeza sehemu za ajira hapa mtaani hali kadhalika kutoa nafasi za kujikimu kimaisha….

Makala haya yameletwa kwako na ruben fm, kwa hisani ya Edmund rice foundation Australia (ERFA) mimi ni mwandalizi wako ledira botere

Read Previous

UCHAFUZI WA HEWA

Read Next

Sheria kuhusu kelele

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular