• July 24, 2024

Sheria kuhusu kelele

 

Wakazi wengi wanoishi mijini hukumbana na tatizo la kelele,kupitia kwa muziki wasauti ya juu unaochezwa kwenye biashara mbalimbali au kelele za watu.

Kaunti ya Nairobi,ambao pia ni mji mkuu hapa Kenya ni moja kati ya miji ambapo wakaazi hukumbana na kelele kupita kiasi. Kelele hizi hushuhudiwa kutokana na muziki wa sauti ya juu kwenye magari,kwenye biashara mbalimbali kama vile vinyozi,wachuuzi,sehemu za burudani,sehemu za kuabudu au hata kelele za redio kwenye ploti.

Hapa nchini, mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira ama NEMA inahusika na kuthibiti kelele miongoni mwa majukumu mengine. Kulingana na katiba,kifungu cha 42(a), Kila mtu ana haki ya kuwa na mazingira safi na yenye afya,ambayo inajumuisha kuishi kwenye mazingira tulivu.

Nimezungumza na wakaazi wa eneo la Mukuru kwa Ruben kubaini iwapo wanaelewa wanapopaswa kuripoti kuhusu uchafuzi wa kelele ama kwa kimombo,noise pollution.

Unaposhuhudia kelele kupita kiasi aidha kutoka kwa biashara,magari,sehemu za burudani au sehemu za kuabudu haswa nyakati za usiku,unapaswa kuripoti wapi?

 

Hapa jijini Nairobi,kuna sheria kuhusu kelele ambayo inajulikana kama The Nairobi City County Nuisance Act ya mwaka 2021. Sheria hii inadokeza kuwa, wakaazi wana haki ya mazingira tulivu, bila kujali aina ya biashara. Kifungu cha 20 cha Sheria hiyo kinasema na nikinukuu: “Mtu hataruhusiwa, katika mtaa wowote au katika duka lolote, eneo la biashara au sehemu yoyote inayopakana na mtaa wowote ambapo umma unakubaliwa; kucheza, kuendesha, kusababisha au kuruhusu kuchezwa au kuendeshwa kwa ala ya muziki, bila waya yaani wireless, gramafoni, amplifier au ala sawa, na hivyo kufanya, kusababisha au kuidhinisha kelele ya sauti kubwa na inayoendelea, au inayorudiwa kuwa kero kwa wakaazi wa majengo yoyote katika kitongoji au kwa wapita njia kwenye mtaani.” Sheria hiyo aidha,inawalinda zaidi wakazi wa Nairobi katika maeneo ya makazi dhidi ya kero za umma ama public nuisance.

Iwapo utaripotiwa kuwa unawapigia watu kelele utachukuliwa hatua. Iwapo ni kwa biashara,NEMA ina mamlka aya kufunga hiyo biashara yako,ukapigawa faini au ukafungwa jela iwapo utakosa kuzingatia ilani ya kupunguza sauti.

Msikilizaji,unashauriwa kuwasilisha malalamiko yako kuhusu kelele kwa NEMA  aidha kwa kuandika barua pepe kwa incidence@nema.go.ke, kwa  kuandika ujumbe kupitia kwa tovuti yao; www.nema.go.ke ama uwapigie simu 0786 101 100. Aidha,unaweza ukapiga ripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu nawe au ukapiga simu kwa maafisa wa polisi kupitia nambari 999.

Ujumbe umeletwa kwako na Ruben FM kwa hisani ya Edmund Rice Foundation Australia.Jina langu ni Tabitha Njambi.

 

 

Read Previous

UFUGAJI WA BLACK SOLDIER FLY

Read Next

Gender roles and social construct

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular