• July 24, 2024

Athari Za Mafuriko Kwa Wanafunzi

Karibu msikilizaji kwenye Makala ya athari za mafuriko kwa wanafunzi hapa mukuru jina langu ni ledira botere.

Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Jumapili hapa JIJINI nairobi ilileta hasara nyingi huku Familia nyingi katika mitaa za mabanda vilivyoko katika kaunti ndogo za Makadara, Starehe na Embakasi Kusini zikikesha  nje na wengine kupewa malazi na majirani zao baada ya nyumba zao kufurika maji.

Walioathiriwa ni wakazi wanaoishi katika vitongoji duni hivi kwani mto ulivunja kingo zake na kuweza kusomba daraja  katika maeneo haya ikiwemo daraja la kayaba na hapa mukuru kwa Reuben, bila kusahau wanafunzi ambao waliathirika pakubwa na mafuriko haya ikiwemo kupoteza vtabu na hata kukosa njia za kuelekea shuleni  kama wanavyonielezea wakaazi hawa….

Hata hivyo ni wazi kuwa baada ya mafuriko haya visa vya maradhi yatokanayo na mvua na baridi nyingi vilidhiirika kwani wanafunzi wengi wameweza kugonjeka homa na mafua…..

Aidha , baadhi ya wakaazi hawa waliweza kutilia kidole cha lawama kwa uongozi duni katika eneo hili la mukuru kwa ujumla na kuweza kuwarai washika dau kuingilia kati……..

Makala haya yameletwa kwako na ruben fm, kwa hisani ya Edmund rice foundation Australia (ERFA) mimi ni mwandalizi wako ledira botere.

 

 

Read Previous

SHERIA MPYA ZA POMBE

Read Next

BAR KARIBU NA SHULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular