• December 19, 2024

UHABA WA MAJI KATIKA ENEO LA MUKURU KWA REUBEN

Maji ni baadhi ya mahitaji muhimu ya kimsingi ya binadamu. Bila maji, shughuli nyingi
muhimu huathirika. Kwa miaka Mingi, serikali baada ya serikali nyingine , hukumbwa na
malalamishi mengi ya ukosefu wa maji katika sehemu nyingi nchini.
Leo tunalivalia njuga swala hili katika mtaa wa Mukuru Kwa Ruben, linalopatikana katika
eneo bunge la Embakasi Kusini. Unapoingia mtaani humo, unakumbana na halaiki ya watu
wakiwa katika shughuli za kutafuta maji. Wengi wao hubeba mitungi nyingi.
Ni sehemu chache tu ambazo maji yanapatikana, hali inayowalazimu Wakaazi wa mtaa huu
kupanga foleni ndefu. Mda mwingi hutumiwa kupanga foleni. Hali hii inalegeza shughuli
zao za kawaida, kama kuosha nguo, maji ya kupika na kuoga hua shida, kwani maji
yanayopatikana ni adimu .
Wanabiashara wa hoteli, pia hawajasazwa katika uhaba huu wa maji. Shughuli zao nyingi
hutegemea maji. Uhaba wa maji ni changamoto kubwa katika shughuli zao za kila siku.
Wakaazi hapa wanaendelea kuisihi serikali kufungua vituo vingi vya maji vinavyoweza
kutosheleza idadi nyingi ya watu katika eneo hilo.
Jack Okenyuro ambaye amekuwa mkaaji wa eneo hilo, kwa miaka Zaidi ya mwongo mmoja
anasimulia.” Shida ya maji inatukera sana katika eneo hili. Watu wamekuwa wengi sana,

licha ya vituo vya maji kuwa chache sana. Sijui serikali kupitia kwa viongozi wake, inaweza
kutusaidia vipi kuhusu swala hili la uhaba wa maji katika mtaa huu.”
Wamama ndio mara nyingi hutafuta maji manyumbani mwao, kwa hivyo, hao ndio huathirika
Zaidi . Mama mmoja mwenye umri wa makamu anasimulia “ Wamama ndio wanao umia
Zaidi kwa ukosefu wa maji. Sana sana, wao ndio hutumika kuyatufuta maji, wanalazimika
kutembea masafa marefu kutafuta maji . Serikali iweze kusikia sauti yetu na iweze
kutusaidia.”
Daraja ya Lungalunga, ilibomolewa na Mafuriko ya mvua, na hivyo, Wakaazi wanalazimika
kutembea ndani ya maji hayo machafu, wanapo anza shughuli ya kutafuta maji. Wanawasihi
viongozi walio wachagua Kuweka haraka ya kutengeneza daraja hio, ili shughuli yao
kutafuta maji irahisishwe.

Maji ni baadhi ya mahitaji muhimu ya kimsingi ya binadamu. Bila maji, shughuli nyingi
muhimu huathirika. Kwa miaka Mingi, serikali baada ya serikali nyingine , hukumbwa na
malalamishi mengi ya ukosefu wa maji katika sehemu nyingi nchini. Hizi hapa ani baadhi ya
sauti zao.

Bilas haka eneo hili linakumbwa na uhaba wa maji. Wanazidi kuisihi serikali Kuweka
mikakati ya kufungua vituo vingi vya maji.Nikiripotia Ruben fm, Jina Langi ni Bob Kau.

Read Previous

Jinamizi La Takataka Katika Mtaa Wa  Mukuru

Read Next

Drainage System in Mukuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular