• December 26, 2024

FAIDA ZA KUCHAKATA TAKA MTAA WA MUKURU

Karibu kwenye kitengo maalum cha ruben fm.Ikiwa leo ni siku njema ambayo maulana ametujalia,ungana nami ledira botere. Sitakuwa peke yangu ila nitaandamana na wezangu……carrilus muye ,martin bunyali na mercy alomba ili kuwaletea ujumbe tuliokuandalia  siku ya leo kwenye  kitengo maalum ambapo tumeangazia faida za kuchakata taka yaani (benefits of recycling waste ) katika mtaa wa mukuru

Taka na nini cha kufanya nazo, ni mojawapo ya tatizo kubwa ya kimazingira yanayowakabili watu wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi jijini Nairobi hivi leo. Huku makazi haya ambayo tayari yanazidi kuongezeka, idadi ya taka ngumu yaani solid waste katika eneo la Mukuru inaendelea kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Kwa ukosefu wa miundo ya kutosha ya usimamizi na rasilimali za kukabiliana na taka, wakazi wanaendelea kukabiliana na matatizo makubwa, kama vile hatari za usafi wa mazingira na mifereji iliyoziba kutokana na kutupwa kwa mabaki ya chakula na makaratasi ambayo huchangia mafuriko makubwa hasa baada ya mvua kubwa na Upepo mkali unapovuma, takataka kutoka eneo la mapipa kawaida hupeperushwa hadi maeneo haya.

Mashirika yasikyo kuwa ya kiserikali kama vile muungano wa wanavijiji wameweza kufanya utafiti kubaini ni kwa kiasi gani taka hizi zinaenea mukuru na ni bayana kuwa takriban asilimia 58 ya wakaazi hulipia baadhi ya utupaji taka, na kuwagharimu kati ya shillingi Ksh 50-80 kwa mwezi na Wahojiwa ambao walisema walitumia huduma ya kuzoa taka walichagua kufanya hivyo kwa sababu wanaona ni salama, na ni ya bei nafuu.

Lakini “hawa wakusanyaji taka hupeleka wapi taka hizi baada ya kuziokota?. Ilionekana wazi kutokana na matokeo hayo kuwa pamoja na shughuli za ukusanyaji zilizopo, wakazi wengi wanaendelea kutupa takataka nyingi badala ya kulipia  Na kwamba hata wakusanyaji wa taka wanapokusanya taka , kuna ushahidi mdogo wa kupendekeza kwamba zitupwe kwa usalama katika eneo lililotengwa la utupaji taka.

Kuzidisha tatizo hilo, baadhi ya maeneo haya ya kutupa taka yamevamiwa na makazi yasiyo rasmi na kinyume chake baadhi ya vibanda vilivyo wazi katika makazi vinatumika kama sehemu za kutupa taka.

Hali kadhalika hapa mukuru vikundi za vijana wameonekana kuwa kwenye mstari wa mbele katika kuchakata taka mfano oasis youth group, biupe youth group, ubuntu youth group ambao wanatumia black soldier fly kuchakata taka na vicco youth group.

 

Tupate wimbo wake msanii beka flavour akieleza shida tunazopitia kutokana na utupaji taka ovyo na jinsi ya kulinda mazingira…..

Read Previous

Drainage System in Mukuru

Read Next

IMPACTS OF VOCATIONAL INSTITUTES IN MUKURU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular