• November 19, 2024

Vijana kama watetezi wa amani ya jamii

Karibu msikilizaji kwenye kitengo maalum cha Ruben fm.Ikiwa leo ni siku njema ambayo maulana ametujalia,ungana nami ledira botere. Sitakuwa peke yangu ila nitaandamana na wezangu……carrilus muye ,martin bunyali na Tabitha njambi ili kuwaletea ujumbe tuliokuandalia  siku ya leo kwenye  kitengo maalum ambapo tumeangazia Vijana kama watetezi wa amani ya jamii katika mtaa wa mukuru

Kuwekeza katika uwezo, uwakala na uongozi wa vijana wanaojenga amani kunaweza kuimarisha uwezo wao wa kushirikiana kuongoza juhudi za amani, na kutumia ustadi wao kukabiliana na changamoto zingine zinazowaathiri haswa katika mitaa ya mabanda ikiwemo mukuru .

Utambuzi huu wa vijana kama nguvu nzuri katika kuzuia na kusuluhisha mizozo na kujenga amani endelevu imepata nguvu kubwa tangu kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kama vile global peace foundation,united nations,peace actions na GIZ, yamekuwa kwenye mstari wa mbele kuhusisha vijana kama kiungo muhimu katika kuimarisha na kulinda amani barani Africa.

Katika eneo la mukuru, vijana pia wamejitokeza ka kutumika kama mfano bora na wakuigwa katika kudumisha amani mfano vikundi kama tujiinue mashinani initiative,vicco na sauti Africa . Kikundi cha sauti Africa kimekuwa ni kikundi bora hapa mukuru kwani wanatumia mbinu ya kuigiza wakitumia vikaragosi na kuweza kuwahamasisha wakazi katika eneo la mukuru kuhusu amani na uridhiano haswa baada ya migogoro.

Read Previous

Undestanding Gen Z behaviour by Denson Moruri

Read Next

VITA AKILINI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular