• November 22, 2024

VIKUNDI VYA USAFI MUKURU

Msukosuko na mabadiliko ya hali ya hewa  ni jambo la kimataifa na linahitaji jamii kutafuta utunzi wa mazingira kwa njia tofauti ili kuitimisha malengo hayo. Njia hizi zitawezesha jamii kuchukulia wajibu na hatua mwafaka kwani ulimwengu unajengwa kupitia jumuiya tofauti  na zenye mipango tofauti tofauti.

Kubadilika kwa hali ya hewa yaani tabia nchi sio tu tatizo la kitaifa mbali pia washika dau tofauti kwenye nchi ambazo zimestawi duniani mfano marekani na yuropa kujiunga na kuleta mabadiliko. Jumuiya hizi ambazo zimestawi hutoa mfano bora  na huweza kutoa  motisha  kwa mataifa yanayostawi na kuweza kuleta mabadiliko.

kujibu maswala haya,vijana katika baadhi ya mitaa ya mabanda ,mashariki mwa jiji la nairobi  mfano  korogocho ambapo mto nairobi unapita na mukuru ambapo mto ngong unapita  wamechukua hatua ya kuhusika na kuongoza katika mipango ya mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.

Eneo la korogocho, ni moja wapo ya mitaa ya mabanda hapa nchini na tunaungana na kikundi cha vijana cha green comb solutions mbao wanatoa mfano bora na wa kuigwa hasa kataika kudumisha usafi katika mto Nairobi  , baadhi ya wahusika kwenye kundi hilo walitufaamisha kwa kina hasa nini kinachowavutia  katika kuulinda mazingira yao………..

Insert……………………………………..

Tukisonga kilomita chache kutoka eneo la korogocho tunakutana na vijana katika eneo la Mukuru ambao pia hawajawachwa nyuma katika kulinda mazingira yao. bwana steven omondi ambaye ni mwakilishi wa ubuntu youth group anatufaamisha kwa kina kupitia mwanahabari wetu carrilus mwangome kuhusu lengo lao kuu huku likiwa ni kuimarisha mazingira kwa kufanya usafi kwenye pembezoni mwa mto ngong…………..

Insert……………………………………

 

Ni bayana kuwa utunzi wa mazingira ni jukumu letu sote na kundi hili la ubuntu ni mfano bora wa kuigwa na kupewa nafasi katika jamii kama kundi la muhimu.jamii ya mukuru pia hawajawachwa nyuma kwani washikadau tofauti  wameonekana kujitokeza kuzidi kuungana na makundi haya ya vijana….

Future Mukiri,mwanajamii wa Mukuru Kwa Ruben anashiriki katika kubadili hali ya hewa kwa kupanda miti eneo la Riverside na mitaa ya mabanda ya mukuru ….

Insert……………

Hali kadhalika, kina mama hawajawachwa nyuma kwani pia nao wamejitosa ulingoni na kuzidi kutilia mkazo umuhimu wa kulinda mazingira …..

Magret wanjiku ambaye ni mwakilishi wa kundi la greenslum innovation hub, pia anashiriki katika mpango wa upandaji miti katika eneo la Mukuru Kwa Ruben akiwa na lengo la kusafisha mto ngong kama inavyojithihirisha kutokana na mazungumzo na mwanahari wetu carrilus mwangome…….

Insert……………………………….

 

Kuhusisha wanajamii wa mukuru , washika dau tofauti ,Kufanya kazi na wanafunzi,wanarika,vyama vya wanarika na wanawake huchangia pakubwa katika kuimarisha mabadiliko hayo ya hali ya hewa kupitia kupanda miti na usafishaji wa mazingira huku hali hii ikiweza kuongeza  matumaini ya kuwa na mabadiliko kwenye tabianchi katika maeneo ya mitaa ya mabanda.

makala haya  yameletwa kwako kwa hisani ya journalist for human rights (JHR) wakishirikiana na HIVOS kupitia Ruben fm. makala haya imeandaliwa na Joseph Oluoch,nami msimulizi wako,ledira botere.

Read Previous

Kangaroo Courts

Read Next

WORLD SAFE ABORTION DAY

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular