• August 20, 2025

Jinsi kuchomwa na nyuki huua

Je,wajua kuwa kuchomwa au kudungwa na nyuki kunaweza sababisha kifo?

Iwapo uko na allergy ya sumu ya nyuki ama bee venom,ukichomwa na nyuki, kinga yako ya mwili itarudi chini, hivyo basi kukusababishia hali inavyoitwa anaphylaxis ambayo ni hatari kwa maisha yako. Anaphylaxis huwa inasababisha kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu,koo na ulimi zinafura na hivyo kupelekea ugumu wa kupumua, moyo wako unapiga kwa kasi na mwishowe unapoteza fahamu.

Pasipo na matibabu ya haraka kama vile matumizi ya EpiPen, anaphylaxis inaweza ikaua kwa dadika chache.

Hata ingawa hauna allergy ya sumu ya nyuki,bado ukichomwa na nyuki wengi kwa pamoja unaweza ukayapoteza maisha yako. Kivipi? Kuchomwa na nyuki wengi kwa pamoja huwa kunafanya sumu nyinyi ya nyuki kuachiliwa kwa wakati mmoja na hivyo kuathiri moyo,figo,maini na damu. Viungo hivi vikifeli kufanya kazi huwa vinasababisha kifo kwa mwathiriwa. Hii huwa hatari hata zaidi kwa watoto na wakongwe.

Wakati mwingine,ukichomwa na nyuki kisha ukose kuzingatia usafi wakati wa kukisafisha kile kidonda,huenda ukapatwa na ugonjwa ambao unaweza ukawa hatari kwa uhai wako.

Tufanyeje tuwe salama?

~Kama uko na allergy ya sumu ya nyuki,hakikisha kuwa ubabeba EpiPen kila wakati.

~Epuka kuchokoza au kuchokora mizinga ya nyuki.

~Tafuta matibabu iwapo umechomwa na nyuki.

Kumbuka;
Kuchomwa na nyuki huwa wakati mwingi kunasababisha uchungu na kufura kwa mwathiriwa, isipokuwa kwa wale ambao wako na allergy ya sumu ya nyuki au unapochomwa na nyuki wengi kwa pamoja.

Read Previous

mbwa wanachinjwa na kuuziwa wakaaazi mukuru kwa Reuben

Read Next

International Youth Day 2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular