FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Katika Shule ya Msingi ya Gatoto, Mukuru kwa Ruben, ambako wakaazi na wanajamii wamejitokeza kwa wingi tangu asubuhi ya leo kuandamana. Maandamano hayo yamechochewa na uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama wa kuagiza umiliki wa shule hiyo kuhamishwa kutoka kwa serikali na kukabidhiwa kwa mmiliki binafsi—hatua ambayo imezua hasira na upinzani mkubwa kutoka kwa jamii.

Wakaazi hao wanataka Shule ya Msingi ya Gatoto isalie chini ya umiliki na usimamizi wa serikali, wakisema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda haki ya watoto wao kupata elimu. Viongozi wa jamii wamesisitiza kuwa shule hiyo ni rasilimali ya umma ambayo imehudumia watoto wa eneo hilo kwa miaka mingi, na kuigeuza kuwa ya kibinafsi kunaweza kuhatarisha maslahi ya jamii na mali ya umma.

Huku hali ikisalia kuwa ya sintofahamu na hisia zikiwa juu, maafisa wa usalama wanaendelea kusimamia maandamano hayo kwa lengo la kudumisha amani na kuzuia ghasia. Waandamanaji, kwa upande wao, wanaendelea kushinikiza mamlaka husika kusikiliza na kushughulikia malalamiko yao.
Story By: Christine Odero