FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Kwa nini mafuriko yanaendelea kuikumba Mukuru kila msimu wa mvua licha ya fedha za kaunti kutengwa kwa ajili ya kukabiliana nayo?
Mukuru ni makazi makazi ya mabanda yaliyo katikati ya jiji la Nairobi, lakini kila msimu wa mvua, wakazi wake hukabiliwa na tatizo la mafuriko. Nyumba hujaa maji, usafiri kutatizika, biashara huathirika na familia kupoteza mali zao. Licha ya serikali ya kaunti kutenga fedha kwa ajili ya kukabiliana na mafuriko, tatizo hili limeendelea kujirudia kila mwaka. Hali hii inazua maswali kuhusu matumizi ya fedha hizo, ujenzi na matengenezo ya mifereji, pamoja na utekelezaji wa miradi ya kudhibiti mafuriko. Je, changamoto ni ukosefu wa miundombinu, mifereji iliyozibwa, upangaji duni wa mji, au kuna pengo katika matumizi na usimamizi wa fedha za umma?
Ungana naye Carrilus Muye akujuze Mengi katika makala yafuatayo.