FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
KUTELEKEZWA KWA WATOTO:
JERUHA LA KIMYA LINALOWEZA KUATHIRI MAISHA YAO
Kutelekezwa kwa mtoto si jambo linaloonekana kila wakati. Wakati mwingine ni hitaji lisilotimizwa, kilio kisichosikilizwa au mtoto ambaye ameacha kuomba msaada kwa sababu anaamini hakuna atakayemsikiliza. Mtoto anahitaji zaidi ya chakula, mavazi na mahali pa kulala. Anahitaji pia upendo, ulinzi, mwongozo, elimu na mtu anayejali hisia zake. Kwa wazazi wanaopitia changamoto za maisha, kuomba msaada si kushindwa kulea. Na kwa jamii, kumwona mtoto mwenye uhitaji kunapaswa kuwa mwanzo wa kumsaidia, si kumsema au kuilaumu familia yake bila kuelewa hali halisi.
Na Carrilus Muye