• November 5, 2026

ERFA STORIES 2026

JUKUMU LETU KUKOMOSHE DHULUMA ZA KIJINSIA

Nyumbani panapaswa kuwa mahali pa usalama, upendo na faraja. Kwa mtoto, nyumba inapaswa kuwa mahali pa kukua bila hofu. Kwa mwanamke, inapaswa kuwa mahali pa kuheshimiwa na kulindwa. Lakini kwa baadhi ya familia, hali ni tofauti. Vitisho, vipigo, kulazimishwa kufanya ngono na aina nyingine za ukatili vinaweza kugeuza nyumba kuwa mahali pa hofu na maumivu. Katika jamii ya Mukuru, kama ilivyo katika jamii nyingine, kupunguza ukatili wa kingono na kijinsia kunahitaji zaidi ya sheria pekee. Kunahitaji hatua kutoka kwa familia, shule, serikali, mashirika ya kijamii na kila mkazi. Swali ni hili: Tunaweza kufanya nini kwa vitendo ili wanawake na watoto waishi katika mazingira salama?

Na Carrilus Muye