• September 6, 2026

ERFA STORIES 2026

 

Wakazi wa Mukuru Wanaelezwa Mara Ngapi Kuhusu Haki na Wajibu Wao Kama Raia?

Mukuru ni mtaa wenye jamii kubwa na yenye shughuli nyingi katikati ya jiji la Nairobi. Hata hivyo, baadhi ya wakazi bado wanakabiliwa na changamoto ya kupata taarifa kuhusu haki zao, wajibu wao kama raia, na nafasi yao katika kushiriki maamuzi yanayoathiri maisha yao ya kila siku.

Ushiriki wa wananchi ni muhimu katika utawala bora, kwani huwapa raia nafasi ya kutoa maoni kuhusu masuala kama bajeti, miradi ya maendeleo, huduma za kijamii, makazi, maji, usafi na miundombinu. Hata hivyo, bado kuna maswali kuhusu iwapo wakazi hupata taarifa kwa wakati, kama fursa za kushiriki zinawafikia wengi, na iwapo maoni yao huzingatiwa na mamlaka husika.

Ungana  naye Carrilus Muye katika makala haya.