FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Kwa Nini Waathiriwa wa SGBV Mukuru Huogopa Kuripoti?
Katika mtaa wa Mukuru, Nairobi, visa vya ukatili wa kijinsia (SGBV) ni changamoto inayowaathiri watu wengi. Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa njia mbalimbali za kuripoti visa hivi, baadhi ya waathiriwa bado huamua kunyamaza. Hofu ya kulipiziwa kisasi, unyanyapaa, kutokuaminiwa, pamoja na ukosefu wa msaada wa kutosha ni miongoni mwa sababu zinazowafanya waathiriwa kusita kuzungumza. Kwa baadhi yao, kuripoti tukio kunaweza kuonekana kama kujiweka katika hatari zaidi, hasa pale mhusika anayesababisha ukatili anapokuwa mtu wa karibu au mwenye ushawishi katika familia au jamii.
Ukimya huu unaweza kufanya visa vya SGBV kuendelea bila hatua kuchukuliwa, huku waathiriwa wakibaki kubeba madhara ya ukatili huo. Kupitia Makala haya yaliyoandaliwa na Carrilus Muye, tunaangazia changamoto zinazowakabili waathiriwa wa SGBV Mukuru, sababu zinazowafanya waogope kuripoti, na umuhimu wa kujenga mazingira salama ambayo yatawawezesha waathiriwa kuzungumza na kupata msaada bila hofu, lawama au unyanyapaa.