FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Katika mtaa wa Mukuru kwa Ruben, eneo la Gatoto, Wakaazi wameungana kwa pamoja katika zoezi kabambe la usafi wa mazingira. Ushirikiano huu wa kijamii unaoendeshwa pamoja na shirika la Akiba Mashinani Trust unalenga kuboresha hali ya afya na mazingira ya eneo hilo. Zoezi hili limepokelewa kwa hamasa kubwa na jamii, huku kila mmoja akijitokeza kwa kauli moja kusafisha mitaro, kuokota taka na kuweka mazingira yao katika hali ya kuridhisha.
Shirika la Akiba Mashinani Trust, ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kuwezesha jamii za mitaa ya mabanda, limepongeza juhudi za wakazi wa Gatoto kwa kujitolea kwao. Viongozi wa zoezi hilo wamesisitiza kuwa usafi wa mazingira ni nguzo kuu katika kuzuia milipuko ya magonjwa na kuimarisha afya ya umma. Ushirikiano huu kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na wakaazi wa eneo hilo umeonyesha mfano wa kuigwa wa jinsi jamii inavyoweza kuchukua hatua za moja kwa moja kujiletea maendeleo.
Huku shughuli hii ikitarajiwa kuendelea kwa wiki kadhaa zijazo katika maeneo mengine tofauti, wakazi wote wanahimizwa vikali kudumisha usafi hata baada ya zoezi hilo kukamilika.
Na Christine Odero