• December 17, 2024

Fact Checks 2021

MICROWAVE NA SARATANI

Ugonjwa wa saratani ambao unashuhudiwa duniani umeonekana kuwa hatari kwa maisha ya binadamu. Watu wengi wanahofia kwamba huenda ugonjwa huo ukapunguza idadi ya watu kwa asilimia kubwa kulingana na takwimu za vifo zinazotolewa mara kwa mara. Baadhi ya watu nchini wanawasiwasi kuwa ugonjwa huo unachangiwa pakubwa na matumizi ya kifaa cha Microwave. Kulingana na wataalam, asilimia sabini ya nyumba nchini zina kifaa hicho. Inasemekana kuwa wakenya wengi wanatumia kifaa hicho kwa maandalizi ya chakula kwani ndio njia inayodhaniwa kuwa rahisi kupika. Katika Makala haya yanayoletwa kwako na Code For Africa kwa ushirikiano na Ruben FM, tunachunguza ili kubaini iwapo matumizi ya Microwave kupika au kuchemsha chakula yanasababisha ugonjwa wa saratani katika mwili wa binadamu…