• December 20, 2024

Harambee Starlets kuwania ubingwa wa dimba la Turkish Women Cup.

Mabingwa wa soka ya wanawake ya Cecafa, Harambee Starlets wamepata mwaliko kuwania ubingwa wa dimba la Turkish Women Cup mnamo Machi 2-11, 2020.

Dimba hilo litaleta pamoja Uturuki, Kenya, Hungary, Venezuela, Hong Kong, Romania, Uzbekistan, Northern Ireland, Turkmenistan na Chile.

Kocha David Ouma anatarajiwa kutangaza kikosi cha kuanza mazoezi hapo Februari 19. Starlets, ambayo imeratibiwa kuanza matayarisho hapo Februari 23 jijini Nairobi, itatumia dimba hilo kujipiga msasa kabla ya mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AWCO ) 2020 kuanza mwezi Aprili.

Vipusa w Ouma watapimana nguvu dhidi ya timu ya humu nchini Februari 29 kabla ya kuelekea Uturuki mnamo Machi 2.

Mashindano ya Uturuki pia yanapatia mshambuliaji mpya wa Besiktas Esse Akida fursa nzuri ya kurejea katika kikosi cha Starlets.

Akida, ambaye alinunuliwa na Besiktas mnamo Februari 17 kutoka nchini Israel, alichezea Starlets mara ya mwisho mwaka 2018.

Draw ya awamu ya kumi na sita bora ya kipute cha kombe la FKF, imefanyika hio jana huku bingwa mtetezi wa kombe hilo, Bandari akitarajiwa kupimana nguvu dhidi ya mwana Sofapaka. Wana benki  KCB watachuana dhidi ya wadosi wa wazito, huku Ingwe Leopards akiratibiwa kupiga na mwana Ushru. Miamba wa soka nchini Gor Mahia watachuana dhidi ya Posta Rangers, Migori Youth wapige dhidi ya Ulinzi Stars, FC Talanta dhidi ya Kariobangi Sharks, Keroka Technical dhidi ya Kisumu All-Stars huku nao Bidco United wakichuana na Fortune Sacco. Michuano hio inatarajiwa kupigwa kati ya tarehe 14  na 15 mwezi machi.

Kwingineko ni kwamba mkondo wa kwanza, awamu ya 16 bora katika  kipute cha UEFA Champions League ulipigwa hio jana, huku Liverpool wakikimbizwa na kukalifishwa ugenini 1-0 na wana Atletico Madrid ya Uhispania. Saul Niguez alipiga bao la kipekee kwa Atletico Madrid katika dakika ya 4 na kuizamisha ndoto ya Jurgen Kloop ya kulitetea taji la kipute hicho.  Kwingineko Kinda Raiyaa wa Norway Erling Braut Halaand alipiga mawili na kuandikisha historia ya kua mchezaji mwenye umri mdogo kabisa kuwahi kupiga mabao 10 katika kipute cha UEFA Champions League. Halaand alipiga mawili katika dakika ya 69 na 77 na kuisaidia Bourusia Dortmund kumwadhibu mwana PSG 2-1 nyumbani. Bao la kufutia machozi kwa PSG ya ufaransa lilipigwa na mchezaji Neyamr jnr katika dakika ya 75. Usiku wa leo kipute hicho kitazidi kunoga huku Atalanta ya Italia ikitarajiwa kuchuana dhidi ya Valencia ya uhispania, huku wana Tottenham Hotspurs chini ya Jose Mourinho wakitarajiwa kupiga dhidi ya RB Leipzig ya ujerumani.

Huenda spurs wakamkosa kiungo Hueng Son Ming mpaka mwishoni mwa msimu baada ya kiungo huyo kuvunjika mkono katia mechi yaligi kuu nchini uingereza dhidi ya Aston Villa. Spurs, na ambao wanazidi kuteswa na majeraha wanamkosa vile vile nahodha mshambulizi Harry Kane,

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Gurdiola amekiri kuwa atasalia katika klabu hio licha ya matatizo yuanayoikumba klabu hio ya uingereza., Pep amezungumza haya katika kikao na wanahabari ambapo aliulizwa hatma yake iwapo marufuku ya kutoshiriki kipute cha klabu bingwa barani ulaya itasimama. Vile vile kiungo mshambulizi wa City, raiyaa wa Uingereza Raheem Sterling hatoondoka katika klabu hio iwapo itashushwa daraja. Manchester City walipigwa marufuku ya kutoshiriki kipute cha UEFA Champions League kwa misimu miwili baada ya kupatrikana na hatia ya kujaribu kukisuka kikosi chao kwa minajili ya kuwahi kombe hilo la UEFA, na vile vile wako katika hatari ya kupokonywa alama na huenda wakashushwa daraja.

Read Previous

 WORLD RADIO DAY 2020 (UMOJA WETU NGUVU YETU.)

Read Next

USALAMA WA WATOTO MTANDAONI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular