• April 23, 2024

USALAMA WA WATOTO MTANDAONI.

 

Teknolojia na matumizi ya mtandao nchini ya mekuwa kwa silimia kubwa huku watumizi wakiendele kuongezeka kila uchao. Kulingana na shirika la muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU, mwaka wa 2019 taifa hili liliandikisha idadi ya wakenya million arobaini na sita laki nane na sabini mia nne na ishirini na mbili wanaotumia mtandao.Takwimu hizo bado hazijadhibitishwa na tume ya mawasiliano nchini CAK japo mikakati imewekwa kuzibainisha. Ni ishara tosha kuwa wakenya wanategemea mtandao kwa shughuli zao za kila siku.

 

Sehemu za kutumia mitandao zinaendelea kufunguliwa maeneo mbalimbali nchini huku kila nyumba ikijitahidi kununua simu ambayo inasaidia kutekeleza shughuli mtandaoni. Hali hii imesababisha Watoto kutambulishwa katika matumizi ya mtandao hasa kwa wale waliofanikiwa kupata nafasi ya kumiliki vifaa hivyo.

 

Kutokana na idadi kubwa ya Watoto wanaotumia mitandao kote duniani, Muungano wa kimataifa wa mawasiliano ulianzisha mradi wa kubuni mbinu ya kuwalinda Watoto mtandaoni dhidi ya madhara yanayotokana na habari potovu. Hatua hiyo imeonekana kukumbatiwa na mataifa mbalimbali Kenya ikiwa miongoni mwake.

 

Mwaka wa 2014 Mamlaka ya mawasiliano nchini CAK iliamua kuanzisha mradi huo nchini wa Be the COP ili kuwalinda Watoto dhidi ya hatari zinazotokana na matumizi ya mtandao.Mradi huo ambao unaendelea unatazamia kutoa habari kuhusu namna ya kuwalinda Watoto wanapotumia mitandao na kuhakikisha wako salama. Mamlaka hiyo hiyo imeshirikiana na washikadau mbalimbali katika harakati za kufanikisha kampeini hiyo kote nchini. Iwapo kampeini hiyo itakumbatiwa na kila mkenya, basi idadi kubwa ya Watoto nchini italindwa dhidi ya hatari za mtandaoni kwani kufikia sasa shule nyingi nchini zinatumia teknolojia katika masomo.

 

Wakenya wanapaswa kuwa mstari wa mbele kufuatilia Watoto kuhusiana nay ale wanayotekeleza mtandaoni. Jukumu hilo halifai kuachiwa Watoto pekee bali sehemu za Watoto kutazama filamu, vibanda vya michezo ya mtandao wa Watoto, shuleni na sehemu mbalimbali. Udhibiti wa hali hiyo utasaidia pakubwa kukuza kizazi kilicho na adabu na chenye kujitambua kwani sheria ya Watoto Nambari 8 ya 2001 inapeana jukumu la uwajibikaji wa wazazi.

mwandalizi ni Martin Kedenge

Read Previous

Harambee Starlets kuwania ubingwa wa dimba la Turkish Women Cup.

Read Next

KALEKWA: FIFA IS A CHEAT, THEY HAVE ROBBED US OUR PLAYER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular