• April 19, 2024

CHOZI LA MTOTO WA KIUME

WHAT A MAN CAN DO, A WOMAN CAN DO BETTER! Ni msemo ambao haukuasisiwa Barani  Afrika lakini umekuwa chanzo cha mabadiliko si haba barani humu.

                 Tangu jadi mtoto wa kike alichukuliwa kama chombo kilichopaswa kutumikishwa na kuleta utajiri katika familia. Hakukuwa na nafasi yoyote ya kujieleza wala kujiendeleza. Naye mtoto wa kiume alibebwa na kuchukuliwa kama dhahabu kwani walifahamu kuwa ataiendeleza jamii na kuleta ulinzi hivyo basi alikuwa na usemi katika jamii. Unyanyasaji wa mtoto wa kike ulikithiri mno, sio kukeketwa tu, bali pia kunyimwa elimu, kuozwa pasipo ridhaa na mengineyo.

                 kupitia unyanyasaji huo wa mtoto wa kike, wapo waliosimama na kupinga vikali na kutafuta usawa wa haki. Lililokuwa janga la jamii, likawa janga la ulimwengu mzima. Vitengo tofauti tofauti vikabuniwa ili kupambana na suala hilo. Leo hii kwa hafla nyingi hotuba za kumpea kipaumbele mtoto wa kike zimekithiri. Serikali nayo imemtengea nafasi za uongozi huku katika masuala ya elimu, alama za kujiunga na vyuo vikuu nchini ziko chini ikilinganishwa na mtoto wa kiume. Wazazi nao hawajaachwa nyuma kumtilia mkazo mtoto huyu. Swali ni je, vipi kuhusu mtoto wa kiume?

Yasikilize makala haya. Mimi naitwa Carrilus Mwangome, nikishirikiana na Caroline Wambere na Dennis Beru.

Read Previous

KALEKWA: FIFA IS A CHEAT, THEY HAVE ROBBED US OUR PLAYER

Read Next

DRAMA GALORE AS KPL TEAMS FAIL TO HONOR BETWAY SHIELD CUP ROUND OF 16 MATCHES

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular