FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
“Utafiti wa vikwazo vya kimfumo kwenye upatikanaji na matumizi ya fedha za makazi nchini Kenya”, yaani kwa lugha ya kimombo Research on systemic barriers towards access and usage of housing finance in Kenya ni
Ripoti iliyotolewa Alhamisi na shirika la Habitat for Humanity wakishikiana na Association of Microfinance Institutions-Kenya (AMFI) na Kenya Mortgage Refinance Company (KMRC)
“Utafiti huu ulijumlisha matokeo ambayo yamewekwa ili kuarifu vipengee muhimu na kuendeleza mipango ya kimkakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu na wadau mbalimbali wa nyumba.
Viwango vya juu vya riba na gharama kubwa za vifaa vya ujenzi vimeorodheshwa kuwa vikwazo vya juu vya upatikanaji wa fedha za makazi kwa vitongoji za kipato cha chini na cha kati.
Kutokana na sampuli ya utafiti huo, asilimia 41 ya wahojiwa wanaoishi maeneo ya mijini walikuwa na nyumba.
Upatikanaji wa fedha za nyumba kwa wakaazi ulikuwa kama ifuatavyo; maeneo ya mijini (asilimia 8), pembezoni mwa miji (asilimia 12), na vijijini (asilimia 16).
Zaidi ya hayo, matokeo yalionyesha kuwa asilimia 56.2 ya watu walioajiriwa rasmi walikuwa na fursa ya kupata mikopo ya nyumba ikilinganishwa na asilimia 29.2 tu kwa watu wasioajiriwa rasmi.
Ripoti hiyo pia iliorodhesha mapato yasiyokuwa thabiti na ukosefu wa dhamana kama sababu zingine zinazozuia Wakenya kupata pesa za makazi.
Haki za umiliki wa ardhi na ufikiaji mdogo wa miundombinu na huduma za kimsingi, kama vile maji, usafi wa mazingira, umeme, barabara na usafirishaji, pia huzuia maendeleo ya makazi na kufanya maeneo fulani kutovutia kwa uwekezaji kulingana na ripoti hiyo.
Utafiti huo ulifanywa katika kaunti 11 zikiwemo Bungoma, Embu, Kajiado, Kakamega, Kiambu, Kilifi, Kisii, Kisumu, Machakos, Mombasa, Nairobi, Nakuru, Nyeri, na Usain Gishu.
Akipokezwa ripoto hiyo Katibu wa Nyumba Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma na Maendeleo ya Miji. Bw. Said Athman kutoka kwake Maurice Makoloo, ambaye ni Makamu wa rais wa Habitat for Humanity Afrika aliahidi kuchukulia kwa umuhimu ripoti hiyo….
Ata hivyo swala la mukuru halikuwachwa nyuma kwani katibu huyo aliweza kutoa mfano…
Nikikamilisha makala haya ni mimi mwandalizi wako ledira botere, ruben fm.