• September 14, 2024

Ganda La Muwa

Ni sauti ya rais William Ruto akizungumza Februari 22, 2023 eneo la Korogocho, kaunti ya Nairobi wakati wa uzinduzi wa tume ya kuangazia usafi wa mito na mazingira kwa ujumla maarufu kama Nairobi Rivers Commission.

Rais alisisitiza ipo haja ya kujumuisha vijana kwa ukamilifu kwenye harakati za kulinda mazingira ikija ni maswala ya uzoaji taka, upanzi wa miti na vilevile utunzaji wa mito kaunti ya Nairobi na taifa kwa jumla.

Eneo la Mukuru linalopatikana kilomita 20 mashariki wa kaunti ya Nairobi …….………..MUKURU AMBIANCE……………………. halijaachwa nyuma  katika harakati  za utunzaji mazingira. Wapo vijana waliojitwika jukumu la kujaribu kusafisha mazingira kupitia uzoaji taka, kupanda miti na vilevile ukulima mjini maarufu kama Urban Farming ambapo wao hutumia mikebe ya plastiki katika shughuli za upanzi mboga za majani.

Stevin Omondi ni mwenyekiti wa kundi la vijana linalofahamika kama Ubuntu ambalo kando na uzoaji taka, wametupilia mbali dhana kwamba kuitwa mkulima yahitaji kumiliki shamba kubwa, hivyo basi wao kama kundi kwa pamoja wametenga nafasi  ndogo ya kipande cha ardhi ambapo wao hupanda mboga kwa plastiki maarufu kama Re-use.

 

Omondi anasema ongezeko la wakaazi wanaozidi kuhamia mjini ndio motisha iliyowasukuma kuanzisha ukulima huo ikizingatiwa kiwango cha chakula na idadi ya watu inakinzana.

 

Kutatua swala uhaba wa chakula haswa upatikanaji wa mboga za kutosha Omondi ana ujumbe huu kwa wakazi.

 

Aidha, ameelezea mpango wa kundi lao  kupanua shughuli zao kwa kununua kipande kikubwa cha ardhi angalau kuzidisha mazao yao, kwani upo umuhimu wa kuwepo kwa mboga hizo kiasi cha haja pamoja na vyakula vingine kutokana na manufaa mengi muno kwa mwili wa binadamu, kauli ambayo mteja wa mboga hizo, Magret Wanjiku ameunga mkono.

 

Lakini ili shughuli za ukulima haswa zile za upanzi wa miti na chakula kunawiri, ipo haja ya utunzaji wa udongo. Ni swala ambalo lipo hatarini kutokana na shughuli za kibinadamu zinatoharibu rotuba ya mchanga kama anavyoeleza Kevin Odongo ambaye ni mwanzilishi wa kundi la Greenslum Innovation Hub lililo mstari wa mbele katika uhifadhi wa udongo eneo la Mukuru.

 

Mwanamazingira huyo ametaka serikali kutilia mkazo sheria za utunzaji mazingira zilizotiwa sahihi, angalau kulingana naye mazingira yatakuwa katika hali bora na yataokolewa kutokana na uharibifu zaidi.

 

Nilipata pia fursa kipekee ya kuzungumza na mwakilishi wadi wa Mukuru Kwa Ruben Scolastica Muthoni kwa njia ya simu kuhusiana na mikakati, wao kama serikali ya kaunti wameweka ili kuchangia katika uhifadhi wa mazingira.

 

Muthoni pia amelezea mpango wa serikali ya kaunti kuanzisha ukulima mjini na miradi ya upanzi wa miti katika shule zote za msingi na upili za umma, mpango ambao ameutaja kama utachangia pakubwa katika wanafunzi kuwa mstari wa mbele  uhifadhi wa mazingira.

 

Msikilizaji hivi unajua kulingana na ripoti ya Julai, 2021 kutoka kwa kamati ya kitaifa ya malalamishi kuhusiana na mazingira nchini NECC, inaashiria kwamba wakenya huzalisha tani 22,000 za taka kila siku huku kaunti ya Nairobi ikizalisha tani 2,400 ambapo kati ya taka hizo asilimia 60-70 huwa ni taka  za kikaboni, asilimia 20 ikiwa ni chuma, huku asilimia moja ikiwa ni kutokana na taka za kimatibabu maarufu kama medical waste.

Vilevile yapaswa ujue iwapo utapatikana na kosa la kuchanganya taka katika sehemu moja, unajiweka kwenye hatari ya kupigwa faini ya shilingi elfu 20 au kifungo kisichozidi miezi sita, kulingana na mswada wa sheria ya usimamizi endelevu wa taka iliyopitishwa mwaka wa 2021.

Yote tisa kumi ni kwamba, ni jukumu lako na langu kuhakikisha plastiki tunazotumia nyumbani au sehemu zetu za kazi zinatumika ipasavyo labda kwa kutilia vyombo ama pia tunaweza panda mboga, vitunguu au mimea mingine kwenye nafasi ndogo iliyo tunakoishi angalau tutakuwa tofauti na wale wanaotumia plastiki na kuzitupa ovyo ovyo, na kwa pamoja tutakuwa tumejikatia tiketi kwa orodha ya watunza mazingira. Ama kweli ganda la muwa la jana, jungu kaona kivuno,

Makala haya yameletwa kwako na Ruben FM kwa ushirikiano na baraza la vyombo vya habari nchini, MCK ukipenda Media Counsil of Kenya.

Mimi ni Moruri Denson, hadi wakati mwingine, kwaheri kwa sasa.

Read Previous

Research on systemic barriers towards access and usage of housing finance in Kenya

Read Next

Kangaroo Courts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular