• December 28, 2024

Kangaroo Courts

Haki ya afya ni haki ya kimsingi ya binadamu iliyohakikishwa katika Katiba ya Kenya. Kifungu cha 43 (1) (a) cha Katiba kinatamka kwamba kila mtu ana haki ya kupata kiwango cha juu cha afya kinachoweza kufikiwa, ambacho kinajumuisha haki ya kupata huduma za afya, ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi.

Mara kwa mara, visa vya dhulma za jinsia na ngono hujitokeza katika jamii, mitaa ya mabanda nchini ikirekodi visa vingi zaidi, japo kwa wakati mwingi huwa haviangaziwi, na waathiriwa kukosa kupata haki, anavyoeleza mwanahabari wetu Mercy Alomba.

Licha ya hakikisho katika kifungu cha 43(1)(a) cha katiba kuhusu haki ya kupatikana kwa huduma ya afya kwa wote, kwa wakati mwingi, haki ya afya  ya uzazi imesalia kizungumkuti kwa waathirwa wa dhulma za kingono na jinsia.

Hili limedhihirika kwenye kikao kilichowaleta wadau mbali mbali pamoja, ili kujadili maswala haswaa ya kupatikana haki kwa waathiriwa wa dhulma za ngono na jinsia, ambapo visa hivi huishia kuambulia patupu, kutokana na kuwepo kwa vikao vya kuvifunikia maarufu kangaroo kourts.

Mike Odhiambo ni wakili wa maswala ya jinsia, anaeleza hizi mahakama nje ya mahakama ni nini.

 

Lakini mbona jamii ishiriki katika kukuza uozo huu?

 

Shirika la Africa Youth trust na action Aid, ni miongoni mwa mashirika yanayofanya kazi katika mitaa ya mabanda kuhamasisha umma kuhusu dhulma za kijinsia na ngono. Winfred Okumu ni mkurugenzi wa Afrika youth trust ayt…..

 

Kangaroo zinaathiri vipi afya ya mwathiriwa

endapo atakosa huduma hitajika baada ya dhulma. Winnie anaeleza zaidi.

 

Kwa upande mwingine mhanga wa dhulma anaeleza baadhi ya athari zinazotokana na kusuluhishwa kwa kesi kinyumbani.

 

 

 

 

Anapendekeza kuzibwe kikamilifu mianya ya kubuniwa kwa vikao hivi.

 

Kwa upande mwingine, mshauri Lydia Ogware anaeleza mwingilio wa mzazi wa mwathiriwa katika kesi anayoshughulikia na sababu za kumnyima bintiye haki ya huduma ikiwemo ya matibabu.

 

Kwa kauli, wanapendekeza mahakama hizi zimalizwe kabisa, kama njia ya kumaliza uozo huu katika jamii na kuhakikisha haki kwa mwathiriwa na wanaotekeleza dhulma wakabiliwe kwa mujibu wa sheria za humu nchini.

Read Previous

Ganda La Muwa

Read Next

VIKUNDI VYA USAFI MUKURU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular