• April 23, 2024

Illegal abortions in mukuru

Karibu msikilizaji kwenye Makala ya upekuzi wa uavyaji mimba zisizo halali wala salama eneo la mukuru, jinalangu ni Ledira Botere.
Licha ya uavyaji mimba kupigwa marufuku katika Katiba mpya, karibu Wakenya 500,000 wanajihusisha na uavyaji mimba usio salama wala halali kulingana na ripoti iliyofanywa na Serikali na mashirika mengine yasikuwa yakiserikali ikiwemo plan international na  African Population and Health Research Center  (APHRC) .

Kinyume na imani iliyozoeleka, kwamba wanawake wasio na waume wanaongoza katika uavyaji mimba, wanawake walioolewa au walio na uhusiano wa muda mrefu wanawakilisha wengi wa wale wanaotibiwa matatizo ya uavyaji mimba, idadi hiyo ikiwa ni asilimia 64 takwimu hii ikiashiria kuwa kati ya wanawake 1000 , wanawake 48 wamehusika kwa utoaji mimba na wenye umri kati ya miaka 15 na 49 nyingi zikiwa zimetokana na mimba zisizotarajiwa.

Nalivalia njuga swala hili ili kuweza kubaini iwapo huduma hii ya uavyaji mimba zisizo za halali zinatokea hapa mukuru na kwa njia zipi.…

naungana naye mwanadada mmoja na kwa usalama wake nimelibana jina lake halisi na kumbandika jina Aisha na akaweza kuniweka wazi hasa ni kipi kilitokea…

Nikiachana na Bi. Aisha naungana na mwanadada mwingine ambaye pia kama bi Aisha na ninalibana jina lake na kumuita Alice ambaye alijaribu kuavya mimba mara mbili mambo yakazidi unga na anazidi kusimulia hasa ni kipi kilitokea..

 

Fauka ya hayo, uavyaji mimba zisizo halali zinafanyika hapa eneo la mukuru huku upatikanaji wa huduma hii ikiwa ya bei rahisi kati ya shilingi elfu mbili hadi shilingi elfu nne na mia tano. Kutokana na uvumbuzi huu , naelekea hadi kwenye sehemu hizi zilizotajwa nikiwa na mpekuzi mwenza bw. John na kuweza kujifanya ningetaka huduma hii ya uavyaji mimba huku nikidai kuwa mchumba wangu ambaye ana ujauzito kama anaweza kupata huduma ya kuavya mimba na ningehitajika nini na je iwapo uavyaji huu ungekuwa na matatizo ni kipi kingetokea,……..

Ata hivyo, adhari zinazotokana na uavyaji mimba huwa nyingi tena sana kama anavyo nielezea daktari…..ambaye ni muuguzi mkuu kwenye hospitali ya ruben centre,………………

Swali ni je iwapo uavyaji wa mimba hapa mukuru unafanyika licha ya kuwa na vitengo tofauti za kuzuia hali hii isiweze kutokea ,nani kazembea kwa kazi yake???
Ni Makala ya upekuzi wa uavyaji mimba usio halali wala salama eneo la mukuru, jinalangu ni Ledira Botere. Ruben fm.

Read Previous

Flooding In Mukuru

Read Next

The pipes Dilemma in mukuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular