• December 20, 2024

Sakaja Super cup

Timu ya creative hands itamenyana na timu ya Nyati fc awamu ya robo fainali kwenye kipute cha sakaja super cup Embakasi kusini baada ya kutoka sare tasa na timu ya dream team hiyo jana.  Kwenye matokeo mengine mukuru combined fc iliirindima Green santos magoli mawili bila jawabu huku real warriors fc ikiduwaza rising city kwa kibano cha magoli mawili kwa nunge, vision fc na gateway zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya kutofungana. Timu zilizofuzu ni Pamoja na reuben united, creative hands, Nyati fc, mukuru combined fc, vision fc, real warriors, kamongo fc na sun city. Awamu ya robo fainali imeratibiwa kusakatwa wikendi hii huku nusu fainali zikichezwa tarehe 15 na 16 november.

Mechi zote za robo fainali zitachezewa ugani vision grounds huku siku ya jumapili kukishuhudiwa mechi kati ya reuben united na mukuru combined mida ya tisa alasiri, kabla ya real warriors kumenyana na kamongo fc mida ya saa saba mchana.

Kwingineko nyati fc itatoana kijasho na fc creative hands CHI siku ya jumatatu saa tisa jioni nayo vision fc imenyane na sun city fc.

 

Na JOHN AMASI

amasijohn56@gmail.com

Read Previous

The pipes Dilemma in mukuru

Read Next

usafi kwa mto ngong

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular