• December 20, 2024

sakaja super cup

Mshambulizi Caleb Abuga alifunga magoli matatu na kusaidia timu yake Creative Hands kufuzu kwenye awamu ya nusu fainali  sakaja super cup embakasi kusini baada ya kutoka nyuma na kuandikisha ushindi wa magoli matatu kwa moja dhidi ya Nyati FC. Magoli hayo matatu yanamweka kwenye orodha ya ufungaji bora zone ya embakasi kusini akiwa amecheka na nyavu mara nane sawia na Alphan Muthoka wa Mukuru Combined. Wafungaji wengine ni pamoja na Christopher Milio wa Reuben United akiwa na magoli matano, Elizaban Okemwa wa Vision FC na magoli manne sawia na mshambulizi wa Shofco Mukuru FC, Brian Apwoka akifunga orodha ya tano bora. Kwingineko vision fc iliibandua Sun City kwa kupata ushindi wa magoli mawili kwa moja na hivyo kufuzu hatua ya nusu fainali.

Mechi babi kubwa ni kati ya mukuru combined ikivaana na dreative hands. Hivi karibuni, timu hizi zimekutana mara mbili huku creative hands ikiwa na ushindi mmoja kati ya mbili. Mukuru combined iliandikisha ushindi wa magoli sita kwa mawili kwenye hatua ya makundi katika kipute cha sakaja super cup huku creative hands ikijibu kupitia kwa taji la ruben fm tournament awamu ya nusu fainali ikiibana kwa goli moja komboa ufe. Je, mwana CHI atarudisha mkono ikikumbukwa kuwa amawmu ya makundi alibebeshwa magoli mengi? Nusu fainali nyingine itakutanisha timu ya kamongo fc, iliyobandua timu ya Real Warriors kupitia kwa matuta ya penalti, na vision fc iliyopenya kwa kuilemaza timu ya sun city magoli mawili kwa moja.

 

#sakajasupercupsemisembakasisouth

Vision FC vs Mukuru Combined FC.

 

Creative Hands CHI Vs Kamongo FC

Na AMASI JOHN.

Read Previous

usafi kwa mto ngong

Read Next

PEACEFUL SPACES ONLINE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular