• September 5, 2024

HEWA CHAFU MUKURU

Kwenye makala maalum,  mwanahabari wetu Mercy Alomba
anaangazia muuaji kimya anayenyemelea mitaa yetu:

Kwa wengi na haswaa wanaoishi katika mitaa ya mabanda, adui huyu asiyeonekana, ana madhara
mengi kwa afya. Ungana naye hadi tamati anapoangazia janga hili linalowakumba walio hatarini zaidi
katika jiji letu, pamoja na baadhi ya hatua ambazo huenda zikaleta afeni katika kukabiliana na tishio hili.

A woman coughing heavily….

Ndivyo maisha ya Margaret Mwenesi mwenye karibia miaka sitini, mkaaji na mfanyi biashara wa kuuza kanga, mayai, nguo za watoto wachanga, shashu miongoni mwa bidhaa zingine kando ya barabara, mtaa waTransormer, eneo bunge la Embakasi Kusini ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku…….

Ila anasimulia changamoto kuu inayomkodolea macho, akihofu usiku na mchana, kikohozi kisicho cha

kawaida.

Kwa miaka, afya yake imekuwa ya kubahatisha anavyonisimulia.

Sawa na wakenya wengine wengi wanaochagua kujinunulia dawa pasi ushauri wa daktari, Mwenesi pia, alifanya vivyo hivyo.

Kufuatia uchunguzi wa daktarI, Mwenesi aliweza kujua chanzo cha kikohozi kisichokoma, ambacho

ananieleza kwa wakati mwingi, huambatana na kufungana kifua.

Lakini anamudu vipi hali hii ikizingatiwa kwa upande wake wa kulia kunaendeshwa biashara ya kuuza

kuni na upande wa kushoto kunachomwa nyama?

Kutokana na maelezo yake, natafuta kujua zaidi kuhusiana na ugonjwa wa pumu, ukipenda Asthma, na daktari Hesbon Maikara kutoka Ruai Family Health ananichorea taswira kamili kuhusu ugonjwa huu.

Lakini Mwenesi anatoa wapi bidhaa za kuuza?

Mtaa wa Eastleigh, ni mojawapo ya mitaa inayoathirika na tatizo la hewa chafu, ikizingatiwa shughuli za

usafiri zilizokithiri, naandamana na Jane hadi mtaa huu, ila anabeba anachokiita uhai wake.

Mbona usitumie mask basi badala ya kuhangaika hivi?

Baada ya shughuli zetu sokoni, tunarejea eneo analofanyia biashara Jane, hapa nikitaka kujua

anavyopata dawa, baada ya kunieleza anatumia inhaler aina tatu

Nikitaka kujua iwapo wanaoishi naye wana ufahamu kuhusu hali yake.

Licha ya unyanyapaa kutoka kwa baadhi ya rafikize, kunao pia wanaomjali……

Lakini mbona wanawake walio na umri uliosonga wanaathirika na ugonjwa huu?

Daktari Maikara anafafanua.

Bila shaka tunajadili swala tata la athari za uchafuzi wa hewa, na ili kuelewa zaidi, napata muda wa

kuzungumza na mtaalam mchunguzi wa viwango vya hewa tunayopumua.

Sammy Wafula Simiyu anaeleza maswala yanayochangia uchafuzi wa hali ya hewa.

Anaeleza wanaoathirika zaidi pia…….

Hali ya Mwenesi, inakaribiana na ya Lily Muthoni, ambaye ameishi na ugonjwa huu kwa zaidi ya miaka ishirinina sita.

Ni dhahiri kwamba kukimu hali hii, sharti mmoja ajikakamue zaidi, ila baadhi wanaolazimika

kutegemeana kwa hali na mali.

Alice pia anatatizika na ugonjwa wa pumu, ila kushiriki inhaler kwake ni jambo la kawaida, kinyume na

Jane na Lily waliosisitiza hawawezi shiriki dawa wao.

Licha ya ufichuzi huu, ananieleza tahadhari anazochukua.

Lakini ni bora kushiriki inhaler daktari?

Kutokana na maelezo ya daktari Maikara, natafuta kujua iwapo walio na ugonjwa wa asthma

wanafahamu hatari ya kushiriki inhaler.

Suzzy ni mkuzaji afya katika jamii kutoka Mukuru kwa Ruben…..

Lakini vipi tutadhibiti uchafuzi wa hewa? Daktari ana ushauri huu.

Msikilizaji, zaidi ya watu milioni mia tatu thelathini ulimwenguni wana ugonjwa wa pumu, kati yao, ni

wakenya milioni nne, huku wataalam wakionya kuhusu uwezekano wa mmoja kupoteza uhai iwapo

hatapata usaidizi wa haraka anapozidiwa na ugonjwa huu. Ni matumaini yangu kwamba kila mmoja

atawajibika ili kuhakikisha tunakabili uchafuzi wa hewa kwa kuzingatia mwongozo wa wataalam ikiwemo

kushiriki upanzi wa miti, kuhakikisha mazingira tunamoishi ni safi, miongoni mwa tahadhari zingine.

Makala haya yameletwa kwako na Ruben FM kwa ushirikiano na Earth Journalism Network EJN.

Nimekuwa mwandalizi na msimulizi wako, Mercy Alomba.

continuous coughing……..fades out…..

.

Read Previous

SHIF COVER

Read Next

UKEKETAJI WA WANAWAKE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular