FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Serikali za kaunti zimetakiwa kuhakikisha mgao wa fedha kwa minajili ya kukuza afya katika jamii zinatumika ipasavyo.
Seneta mteule Veronica Maina ametoa changamoto kwa magavana kuhakikisha hapashuhudiwi ubathirifu wa pesa katika serikali zao, katika jitihada za kuinua viwango vya kuafikiwa afya kwa kila mkenya. Maina ametoa changamoto hii wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa huduma za upasuaji wa ulemavu wa mdomo maarufu cleft lip, na hospitali ya BelaRisu bila malipo, ili kufaidi wengi ikizingatiwa hugarimu kati ya shilingi alfu 300-350 kumfanyia mwathiriwa mmoja upasuaji.
Huwa ni furaha kwa kila anayebarikiwa na mtoto, ila mambo huwa visivyo haswaa mmoja anapopata mtoto aliye na ulemavu wowote ule.
Ndivyo hali ilivyokuwa kwa familia ya Simon Munene, mzaliwa wa Nyeri. Anaeleza kupata mwana aliye na ulemavu wa mdomo kulileta maswali haba bila majibu.
Munene anaeleza changamoto Zaidi walizokumbana nazo kama familia.
Familia hii ni mojawapo tu ya familia zinazohangaika katika kutafuta tib ana jawabu kwa wanao waliozaliwa na ulemavu wa mdomo, daktari Martin Kimani, mtaalam wa upasuaji wa urekebishaji wa ulemavu wa mdomo katika hospitali ya BelaRisu iliyo Ngara, hapa Nairobi akieleza hali hii ni ya kawaida na inaweza kushughulikiwa.
Alieleza haya wakati wa maadhimisho wa mwaka mmoja wa utoaji huduma kwa waathiriwa wa ulemavu huu, na kufichua watoto alfu saba wamenufaika na huduma hii, japo anaeleza changamoto kadhaa wanazokumbana nazo katika utoaji huduma.
Seneta mteule Veronica Maina akiwataka wazazi walio na watoto wenye ulemavu wa mdomo kuwasiliana na hospitali hii, kupata usaidizi.
Takriban watoto 2000 huzaliwa na ulemavu wa mdomo nchini kila mwaka, huku wachache wakibahatika kupata upasuaji ufaao kurekebisha hali hii, kwa mujibu wa daktari Maina, huku mwenzake, Dakta Khan, akisisitiza kujitolea kuhakikisha wengi wananufaika na wakfu huu.