FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Mnamo saa tisa usiku wa tarehe 23 Septemba 2025, moto mkubwa ulizuka katika eneo la Paradise, Sinai, Makadara. Chanzo chake kilikuwa mabishano ya kifamilia ambayo yaligeuka kuwa janga. Moto huo uliathiri familia 274 ambazo zilipoteza makazi na mali zao zote, huku watu wawili wakipoteza maisha.
Magari matatu ya zimamoto yalipelekwa eneo la tukio na hatimaye kufanikisha kuuzima moto. Hata hivyo, wakazi walilalamikia changamoto zilizochelewesha juhudi za uokoaji, ikiwemo gari la kwanza kukosa maji ya kutosha na barabara duni ambazo zilizuia upatikanaji wa haraka. Kwa maoni yao, hasara ingeepukika iwapo huduma za dharura zingekuwa bora na miundombinu iboreshwe.
Kwa sasa, manusura wa mkasa huo wamesalia bila makazi na wanategemea msaada wa dharura. Mwakilishi wa Mbunge wa Makadara, kwa kushirikiana na viongozi wa eneo hilo na shirika la Hatua kwa Hatua CBO, wameanzisha mgao wa chakula kwa familia zilizoathirika. Pia, wameahidi kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Majanga ili msaada zaidi utolewe kwa familia zote 274.
Tukio hili limedhihirisha udhaifu katika maandalizi ya dharura, na limeibua haja ya kuimarisha huduma za zimamoto, kuboresha barabara za mitaa ya mabanda, pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu usalama wa moto. Aidha, familia zilizoathirika zinahitaji msaada wa muda mrefu ili kurejea kwenye maisha yao ya kawaida.
report by Alice