• December 20, 2024

habari zetu za spoti

Hujambo msikilizaji wangu na natumai umeshinda vyema karibu kwenye habari zetu za spoti awamu ya
mchana ukiletewa nami nahodha wako Amasi John aka beki nambari tatu mgongoni.
Tukianza na taarifa za raga ni kwamba timu ya Namibia itakua inatafuta ushindi wake wa kwanza dhidi
ya mwenyeji Ufaransa kwenye kundi A katika michuano ya rugby world cup 15' zinazoendelea nchini
Ufaransa. Timu hizi zimekutana mara mbili katika world cup huku Namibia wakipoteza mechi zote.
Ushindi wa Namibia utakua wa kwanza dhidi ya Ufaransa wakiwa wamekutana mara tatu. Hiyo jana
Italia ilipata ushindi wa alama 38 -17 dhidi ya Uruguay na kupaa hadi kidedeani katika kundi A.
Aliyekua kiungo mkabaji wa Harambee Stars na mchezaji wa CF Montreal kwenye ligi ya MLS, Victor
Wanyama alijumuishwakwa kikosi cha kwanza baada ya kutumika kama mchezaji wa akiba kwa muda
wa miezi miwili, dhidi ya timu ya FC Cincinnati kwenye mechi iliyochezwa leo asubuhi. Wanyama
alicheza dakika 87' kabla ya kuondolewa uwanjani huku akiwaa amecheza jumla ya mechi 23 msimu huu
na kuanza kwenye kikosi cha kwanza mechi 20 . Mechi hiyo iliishia sare ya bao moja huku CF Montreal
kufikia sasa ikiwa nafasi ya 8 na alama 37 baada na mechi 29.
Kwenye habari zingine, mechi za awamu ya kufuzu katika kipute cha taifa bingwa bara Afrika upande wa
akina dada kitakichofanyika nchini Morocco mwaka ujao, kumeratibiwa mechi tatu kutoka nyanja tofauti
huku timu ya kina dada ya Guinea ikiikaribisha timu ya Mauritius saa kumi na mbili jioni, Guinea Bissau
itavaana na Congo saa kumi na mbili unusu na mechi ya mwisho ikikutanisha Gambia na Namibia
kuanzia saa mbili usiku.
Na kwenye rubaa za kimataifa, hapo jana kumeshuhudiwa mechi kutoka nyanja tofauti katika ligi ya
championship uingereza huku blackburn wakipata kibano cha 1-3 dhidi ya sunderland, huddersfield na
stoke city zilitoka sare ya kufungana magoli 2, timu ya millwall ikapata ushinda wa magoli 3 kwa nunge
dhidi ya timu ya rotherham, huku Watford ikitoana kijasho na west brom kwa kufungana magoli 2 na
Norwich city ikapoteza mikoni mwa Leicester city 2-0
Na tukiangazia matokeo ya mechi zilizogaragazwa hiyo jana katika kipute cha klabu bingwa bara ulaya ,
almaarufu UEFA CHAMPIONS LEAGUE, klabu ya arsenal ilianza vyema katika kampeni za mechi hizi kwa
kumlaza mpinzani wake PSV magoli manne kwa nunge ugani emirates. Mshambulizi Bukayo saka
aliweka arsenal kifua mbele katika dakika ya 8, dakika 12 baadaye saka alimpa pasi nyerezi kwa Leandro
trossard na kucheka na nyavu kufanya mambo kuwa mawili. Gabriel jesus alitia kimyan bao la tatu
dakika 7 kabla ya mapumziko na kuzika matumaini ya psv kupata ushindi, huku nahodha martin
odegaard akipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza kwa kufunga goli la 4 dakika ya 70. Arsenal mara
ya mwisho kushiri kwenye kipute hiki ilikua ni mwaka 2017. Kwenye matokeo mengine, .timu za
Galatasaray na Copenhagen zilitoka sare ya magoli mawili huku goli la dakika 94+ lake Jude Bellingham
lilisaidia timu ya real madrid kuokota alama zote tatu na kuilaza timu ya union berlin 1-0, Bayern
munich 4-3 manchester united ugani allianz arena, braga 1-2 napoli, real Sociedad 1-1 inter milan, sevilla
1-1 lens.
Na tuikamilishe habari za spoti kwa kuangazia ratiba za mechi za kuwania kombe la Europa league
ambapo timu ya Liverpool ya uingereza itakua mgeni wat imu ya LASK kuanzia saa mbili kasorobo, huku
Bayern Leverkusen ikimkaribisha hacken saa mbili kasorobo, brighton & hove albion vs aek, ajax
ikichuana Marseille zote zikiratibiwa kuanza saa nne usiku. Bingwa mtetezi wa kombe la Europa
conference league westham atakua anamkaribisha TSC nyumbani London stadium ikianza saa nne usiku.

 

Kufikia sasa nalikunja jamvi la spoti, nimekua nahodha wako Amasi John aka beki nambari tatu
mgongoni kua na jioni njema.

Read Previous

DUMPING IN MUKURU

Read Next

State Of Roads In Mukuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular