• September 11, 2024

kipute cha Sakaja Super Cup

Mechi zinazidi kunoga kila uchao kwenye kipute cha kuwania taji la Sakaja Super Cup. Timu zinazidi kujizatiti iwezekanavyo kuhakikisha kuwa zinang’ang’ania nafasi ya kuwakilisha jimbo lake kwenye fainali hizi zitakazofanyika mwanzoni wa mwezi desemba mwaka huu.

Wikendi iliyopita kumeshudiwa mechi kabambe kutoka nyanja za vision na ruben grounds katika jimbo hili la Embakasi Kusini, huku mechi za mwisho katika makundi zikifikia tamati siku ya alhamisi.

Timu ya City Foxes iliandikisha ushindi wa magoli matatu kwa moja dhidi ya mpinzani wake Gateway hiyo jana, Kamongo FC ikiibana Shofco Mukuru magoli mawili kwa nunge. Pipeline FC, baada ya kupokea kibano kikubwa cha magoli manne kwa mawili mikononi mwa mwanacreative hands CHI, wikendi iliopita, iliduwazwa na mwanamukuru Combined kwa kufungwa magoli mawili kwa moja, nayo Rising City ikikalifishwa na Vision FC goli moja kwa nunge.

Siku ya jumamosi, timu ya Cyprus ilipoteza goli moja bila jibu mikononi mwa fc barca, dreamteam ikichabanga green santos matoli mawili kwa moja huku bokastars wakinyukwa magoli matatu kwa moja na Corinthians, huku lengends wakiandikisha ushindi mwembamba wa goli moja bila jawabu.

Awamu ya makundi itafikia ukingoni juma hili katika majimbo mengine huku kukisubiriwa ratiba ya robo fainali kutolewa na kutafuta mwakilishi kutoka magatuzi yote kumi na tano.

Hiyo kesho, Bokastars itavaana na reuben united fc mida ya saa kumi alasiri ugani vision grounds, nayo Corinthians ikabane koo na legends fc saa kumi alasiri ugani reuben grounds, katika zone A. katika zone D, Cyprus fc na shofco mukuru fc itatoana kijasho ugani reuben grounds saa nane mchana, nayo kamongo fc ikamilishe mechi yake ya makundi na timu ya sun city vision grounds saa nane mchana. Siku ya alhamisi, ugani vision kutashuhudiwa mechi mbili za makundi tufauti huku mwanacreative hands akijaribu nafasi yake ya kufuzu hatua ya robo fainali ikikabana koo na dream team fc zone B, nazo timu za gateway fc na vision fc zikikalisha mechi zao za makundi. Katika uga wa reuben grounds, real warriors na rising city zikipimana nguvu mida ya saa nane mchana kisha baadaye kushuhudiwe mechi babi kubwa ikishirikisha timu za green santos na mukuru combined mida ya saa kumi alasiri.

 

Na Mwanaspoti JOHN AMASI.

 

Read Previous

POOR DRAINAGES IN MUKURU

Read Next

Unveiling the Struggles of insecurity in Mukuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular