UFISADI NA UNYAKUZI WA ARDHI MUKURU KWA NJENGA.

Ni sauti za unyonge za baadhi tu ya waathiriwa wa ubomozi katika eneo la Sisal, wadi wa Mukuru kwa Njenga, kaunti ndogo ya Embakasi kusini kaunti ya Nairobi, ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa barabara ya Catherine Ndereba Novemba mwaka wa 2021.

Kilichofuata ni dhulma za kingono na unyanyasaji uliolenga haswaa kina mama wasio na waume na kina mama waseja, baadhi wakidhulumiwa kingono machoni pa watoto wao.

Jitihada zao kutafuta haki ziliishia uvumbuzi mwingine, wakibaini ubomozi ulifuatia mzozo wa umiliki wa kipande hicho cha ardhi baina ya kampuni ya Orbit Chemicals Limited na maskwota wanaodai kuishi eneo hilo tangu miaka ya 1952.

Lakini mzozo huu wa kipande cha ardhi cha ekari 95.2 ulianza vipi? Mzee kwa jina Ochieng kutoka eneo hilo ananipa historia fupi.

Tangu ununuzi wa kipande hiki cha ardhi mwaka wa 1985 na kampuni ya Orbit kutoka benki iliyomilikiwa na serikali ya National Bank, kampuni hiyo imekuwa kwenye kesi aidha na serikali au wenye nyumba wanaodai kuwa maskwota, na licha ya mahakama kuamua mara kadhaa kwa faida ya kampuni ya Orbit, amri ya kurejeshewa fedha zake kulingana na gharama ya sasa imesalia tu katika kumbukumbu za mahakama, kampuni hiyo ikiendelea kuhesabu hasara.

Lakini hili lilitokea vipi?

Mzee Ochieng, ananifafanulia kuzungumkukti hiki, akieleza asili ya wapangaji wanaodai kumiliki eneo hili.

Mwenzake ninayempa jina Joel, anaendeleza na maelezo haya, akinifuchulia kuwa serikali, kwa wakati fulani, ilipeana ardhi hiyo kwa watu binafsi ili kuiendeleza kwa kilimo na ujenzi wa kampuni ambazo zingebuni nafasi za ajira kwa waliokuwa wakiishi karibu na maeneo hayo. Hata hivyo, kulikuwa na masharti kwa waliopewa.

Ochieng akirudi nyuma kiasi, kunieleza serikali ilivyouzia kampuni ya Orbit shida zake.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa masaibu kwa kampuni ya Orbit.

Lakini mwaka 2021, Maisha ya wengi yalibadilika, wasijue la kufanya.

Serikali ikidaiwa kushiriki katika kuhangaisha raia wake.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kesi ndefu kortini, japo hawajapoteza matumaini.

Kilele cha vitisho vya kubomolewa kilikuwa mwaka 2021 Novemba.

Napata kuzungumza na mmoja wa waathiriwa wa ubomozi huo,

anayejitambulisha kwa jina Jacky.

Nikitaka kujua alivyopata umiliki wa kipande alichokuwa amejenga nyumba ya orofa tatu kwa minajili ya kukodisha kwa makaazi Pamoja na eneo la kibiashara.

SACCO anayodai iliuzia wengi kipande cha ardhi, hata hivyo haipo tena, na jitihada za kupata Habari zaidi kuihusu zinakosa kuzaa matunda.

Jacky anasimulia kupokea vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa

watu anaodai walitumwa na mabwanyenye waliokuwa wakimezea eneo hilo mate.

Hatimaye walitimiza kiapo na vitisho vyao vya mara kwa mara.

Kana kwamba uharibifu wa kwanza haukuwaridhisha, walirudi tena.

Jacky anadai kudhalalishwa katika jitihada zake za kutafuta haki kwa ushirikiano na dadake na waathiriwa wengine.

Lakini Jacky na wenzake wakiendeleza mchakato wa kutafuta haki, nataka kujua iwapo wana stakabadhi zozote za kuonyesha wanamiliki kipande hicho cha ardhi.

Kwa upande mwingine, baada ya jitihada za kumtafuta mmiliki wa kampuni ya Orbit ananielekeza kwenye taarifa kuhusu kipande hiki kinachozozaniwa. Natambua kwamba kipande hicho cha ardhi chenye ekari 95.2 kiligawanywa, huku ploti 626 zikiunuliwa, kati yazo 446 zikahamishiwa kwa wamiliki wapya,  705 zikisalia chini ya Orbit Chemicals.

Licha ya hatua hiyo kuchukuliwa, Sachen Chandaria, mmiliki wa Orbit Chemicals hajaweza kikutwaa ili kukiendeleza, akisisitiza maskwota hawaruhusiwi kukiuza.

Maswali zaidi yakiibuliwa, kuhusiana na sheria za umiliki na ununuzi wa ardhi hapa Nairobi sawa na maeneo mengine nchini, ikizingatiwa baadhi ya waathiriwa wanadai kununua sehemu ya kipande hicho cha ardhi.

Msikilizaji, usikose kuungana nami nikikuletea awamu ya pili ya makala haya, wakili Gloria Lucky, ambaye ni mtaalam wa maswala ya ardhi katika mahakama kuu hapa nchini Kenya, akieleza mchakato wa ununuzi wa ardhi, na baadhi ya vigezo ambavyo wengi hukosa kutekeleza, na kuchangia katika kuenea kwa ufisadi na unyakuzi wa ardhi nchini.

Hujambo na karibu kwenye awamu ya pili  ya jasusi kuhusu unyakuzi na ufisadi katika sekta ya mashamba nchini, nikiangazia kipande cha ardhi cha ekari 95.2 ambacho umiliki wake umesalia kizungumkuti, ikizingatiwa kampuni ya Orbit Chemical Industries Limited inadai umiliki wake, huku baadhi ya maskwota wakidai pia umiliki wa kipande hicho cha ardhi.

Jacky ni mmoja wa waathiriwa wa ununuzi wa kipande cha ardhi, akieleza masaibu yaliyomkuta kutokana na kipande cha ardhi kilichonunuliwa na dadake kutoka kwa sacco.

Kwa upande mwingine, afisa mkuu mtendaji ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Orbit Chemical Industries Limited Sachen Chandaria akidai pia kuuzia baadhi ya maskwota sehemu ya ardhi hiyo inayozozaniwa, baada ya serikali kumpa hati miliki za ardhi.

Napata kufanya kikao na wakili Gloria Lucky, ambaye ni mtaalam wa maswala ya ardhi katika mahakama kuu hapa nchini Kenya.

Ananieleza mchakato wa ununuzi wa ardhi, na baadhi ya vigezo ambavyo wengi hukosa kutekeleza, na kuchangia kuenea kwa udanganyifu katika sekta ya ardhi.

Anaeleza zaidi

Kwa upande mwingine, anaeleza haja ya kufanya uchunguzi wa kina unapaswa kufanywa na mnunuzi wa shamba.

Vile vile wakili anaeleza baadhi ya vitu mnunuzi anapaswa kufanya asije akapokonywa shamba alilonunua kihalali.

Kutokana na maelezo ya wakili Gloria, napata fursa ya kuzungumza na Roselyne Asena, mmoja wa wanaharakati katika eneo bunge la Embakasi Kusini anayejihusisha na kuhamashisha jamii kuhusu maswala muhimu ikiwemo umiliki wa shamba katika mitaa ya mabanda.

Anachora taswira ya wanapoingilia katika kuelimisha raia haki za umiliki wa shamba.

Akieleza wengi hawajui haki ya kuhamishwa kutoka kipande cha ardhi licha ya kutokimiliki.

Hata hivyo, anatoa tahadhari kwa wanaharakati wenza, haswaa ifikiapo maswala yanayoihusu serikali.

Usemi wake unatiliwa mkazo na shirika la Transparency International, kwenye mwongozo wake katika jitihada za kumaliza ufisadi katika sekta y a ardhi nchini, ikizingatiwa kwa wakati mwingi wengi wameathirika wakati wa mchakato wa ununuzi wa ardhi, haswaa wanapolazimia kutoa kitu kidogo, ili kufanikisha ununuzi huo, japo wengi huishia kupoteza mamilioni ya pesa, kwa kutofuata mwafaka wa ununuzi wa ardhi nchini.

Hadi wakati huo, nimekuwa mwandalizi na msimulizi wako Mercy Alomba.

Read Previous

dhuluma za kijinsia

Read Next

Bridge of Hope: OCS Noor’s Journey in Rebuilding Communities

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular