• December 19, 2024

Fact checks 2020

Kasumba Za Unyonyeshaji

Agizo kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
watoto yaani UNICEF ni kuwa mtoto anapaswa kunyonyeshwa kwa miezi ya kwanza sita
mfululizo na kuendelezwa hadi miaka miwili au zaidi pamoja na vyakula mbadala. Lakini je,ni
kwa nini akina mama wengi wanashindwa kufuata kanuni hii kwa kina? Pamoja na sababu
zingine ni kuwa, akina mama wengi hufuata imani potovu za kimila na kasumba kuhusu
unyonyeshaji.Ni kasumba zipi ulizosikia kuhusu unyonyeshaji,na je,unadhani kuna ukweli
wowote katika kasumba hizo?