• December 26, 2024

Fact checks 2020

Men At a Higher Risk of Covid

Wizara ya afya nchini Kenya imekuwa kwa kiwango kikubwa ikiwarai wakenya kuvalia maski ama
barakoa ili kusaidia kupambana na msambao wa homa kali ya mapafu ya korona. Jambo ambalo
wanaume wengi wanaonekana kulipuuzilia mbali hili likidhibitishwa na waziri wa afya Bwana Mutahi
Kagwe katika hotuba mbalimbali kwa taifa. Mwanahabari wetu Jeremiah Mutua alitembea sehemu
mbali mbali za Mukuru ili kubaini ukweli iwapo wanaume wengi wanavaa ama hawavai maski
ikilinganishwa na wanawake na baadae akamtembelea Muuguzi Elijah Gachuki ili kujua kwanini kuna
maambukizi mengi ya corona kwa wanaume kuliko wanawake.