FALSE: Photo does not show the drought situation in Embolioi, Kajiado County, in October 2022
Ya mgambo ikilia ina jambo basi sasa imeshalia na mdharau biu hubiuka mwenyewe. karibu katika makala ya NDOA NDOANA tukiangazia maisha ya ndoa , yaani utamu ndani ya uchungu. Sisemi kitu.
Tukiyafungua macho na kutazama kwa undani hali ya ndoa miaka ya jadi, ndoa iliheshimika, ikatunzwa na watu wakaienzi. Tunapopiga jicho vitabu vya dini yayo hayo yanasisitizwa. Ndoa imekuwa kama biashara, ama nifananishe na siasa hasa za taifa la Kenya, lakini haya yanaishia tu hapa. Watu wanaingia watakavyo saa yoyote, wakati wowote kama vile mja anavyoingia msalani. Kwa maana nyingine ndoa imepoteza maadali na misingi yake thabiti. Tazama vile vijana wanavyokimbilia ndoa, utadhani kuna raha huko, badaaye wanatoka wakiwa na makovu ya moyo na hapo ndio utasikia “ALL MEN ARE DOGS” wengine watasema “ALL LADIES ARE THE SAME”. Wakati wengine wanazikimbia huku wengine wanazikimbilia.
Usikose kusikiliza makala haya. Mwelekezi ni Thomas Odhiambo, mimi naitwa Carrilus Mwangome nikishirikiana na Bosco Kathima.